Upatikanaji viungo

Breaking News
Ijumaa, Desemba 06, 2024 Local time: 04:44
VOA Direct Packages

Wachimba migodi 14 wafariki kwenye mgodi wa dhahabu Sudan


Picha ya maktaba ya mgodi
Picha ya maktaba ya mgodi

Serikali ya Sudan imesema leo kwamba takriban wachimba migodi 14 wamekufa baada ya mgodi wa dhahabu kuporomoka kakazinini mwa nchi.

Tukio hilo linasemekana kutokea baada ya milima inayozunguka mgodi huo wa Jebel Al Ahmar karibu na mpaka wa Misri, kuporomoka Alhamisi jioni, kwa mujibu wa taarifa fupi kutoka kampuni ya madini ya Sudan.

Wachimba migodi wengine 20 wamejeruhiwa na kupelekwa katika hospitali ya karibu. Kulingana na ripoti iliyochapishwa Alhamisi na shirika la habari la serikali la SUNA, shughuli za uokozi za kuwatafuta watu waliokwama chini ya ardhi zinaendelea.

Mashuhuda walionukuliwa na SUNA wamesema kwamba wachimba migodi walikuwa wakitumia mashine zenye nguvu kutafuta dhahabu ndani ya mgodi huo ambazo zilisababisha kuporomoka.

Vyanzo vya kiusalama vimetajwa na SUNA vikisema kwamba huenda kuna wafanyakazi waliokwamba kwenye maji yaliopo ndani ya mgodi.

XS
SM
MD
LG