Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumatano, Mei 29, 2024 Local time: 11:39

Mahakama yaruhusu mume wa mwanariadha Agnes aliyeuawa kukaa rumande zaidi


Hayati Agnes Tirop (Photo by MUSTAFA ABUMUNES / AFP)
Hayati Agnes Tirop (Photo by MUSTAFA ABUMUNES / AFP)

Mahakama ya Kenya Jumatatu iliwaruhusu polisi kumshikilia mume wa mwanariadha wa mbio ndefu, Agnes Tirop, kwa siku 20 kufuatia mauaji ya Agnes, kituo cha habari cha KTN kiliripoti.

Mume wa Tirop, Ibrahim Rotich, alishtakiwa kwa tuhuma za mauaji wakati alipofikishwa mahakamani kwa mara ya kwanza huko a Rift Valley katika mji wa Iten, karibu na nyumba waliokuwa wakiishi.

Polisi waliiambia mahakama kwamba watatumia muda huo kukamilisha uchunguzi na kuendeleza zoezi hilo zaidi kwa mshukiwa kubaini kama ana uwezo kamili wa akili kusimama mahakamani.

Maafisa wa upelelezi walimkamata Rotich siku ya Alhamisi katika mji wa pwani ya Mombasa, wakisema alikuwa akijaribu kukimbia nchini.

Siyo Rotich, wala wawakilishi wake waliyotoa maoni yoyote ya umma juu ya kesi hiyo.

XS
SM
MD
LG