Upatikanaji viungo

Breaking News
Ijumaa, Mei 24, 2024 Local time: 09:40

Wanaraiadha wa Afrika waendelea kutamba katika Olimpiki.


Mwanariadha wa Afrika Kusini Wayde van Niekerk akichukua nafasi ya kwanza katika raundi ya kwanza ya michuano ya mkita 400 kwa wanaume. REUTERS/Phil Noble
Mwanariadha wa Afrika Kusini Wayde van Niekerk akichukua nafasi ya kwanza katika raundi ya kwanza ya michuano ya mkita 400 kwa wanaume. REUTERS/Phil Noble

Wanariadha wa Afrika wameendelea kuonyesha umahiri wao katika riadha huku bara hilo likishuhudia kuondolewa katika michezo mingine

Wanariadha wa Afrika wameendelea kuonyesha umahiri wao katika riadha huku bara hilo likishuhudia kuondolewa katika michezo mingine ambapo katika upande wa riadha wanaume katika mbio za mita 3000 kuruka viunzi waafrika waling’ara baada ya Soufiane El Bakkali wa Morocco kutwaa taji la Olimpiki katika mbio za mita 3,000 na kuchukua medali ya dhahabu. Alikuwa mshindi wa kwanza wa medali hiyo wa Moroco kwenye michezo yote tangu Hicham El Guerrouj mnamo mwaka 2004.

El Bakkali, mwenye umri wa miaka 25, alikuwa mbele kwa dakika 8 sekunde 08 dhidi ya Mwethiopia Lamecha Girma na Mkenya Benjamin Kigen ambaye amechukua nafasi ya Mkenya Conseslus Kipruto ambaye hayupo mwaka huu. Morocco imekomesha utawala wa Kenya katika mbio ndefu baada ya mataji tisa mfululizo ya Olimpiki tangu mwaka 1984.

Kwa upande wa wanawake katika mbio za mita 5,000 bingwa wa dunia aliyetawala mara mbili Mkenya Hellen Obiri aliishia kupata medali ya fedha, kama mwaka 2016. Alitumia dakika 14 sekunde 38, akimaliza wa pili mbele ya Muethiopia Gudaf Tsegay.

Nafasi ya kwanza ya medali ya Dhahabu ilikwenda kwa mwanamke Mholanzi ambaye ni mzaliwa wa Ethiopia Sifan Hassan, akitumia dakika 14:36. Alizaliwa nchini Ethiopia, na Sifan Hassan aliwasili Uholanzi kama mkimbizi mnamo mwaka 2008.

Mkimbiaji wa Ivory Coast Marie Jose Ta Lou anatabasamu tena katika mbio za nusu fainali ya wanawake za mita 200 baada ya kumaliza katika nafasi ya kwanza akitumia sekunde 22.11 .

Sasa akiwa ameingia fainali mwanadada huyo atajaribu kunyakua medali katika fainali hizo, Lou alimaliza katika nafasi ya 4 wiki iliyopita katika mbio za mita 100.

Wanawake wengine wa Kiafrika waliofuzu kwenye fainali za mita 200, ni wanariadha wawili wa Namibia Beatrice Masilingi na Christine Mboma, wote wenye umri wa miaka 18. Mboma, alivunja tena rekodi ya dunia ya vijana lakini pia rekodi ya Afrika. Alimaliza mbio zake kwa sekunde 21.97.

Kwa upande mwingine mwanariadha Aminatou Seyni, kutoka Niger aliondolewa katika mashindano baada ya kumaliza akiwa katika nafasi ya 5 na sekunde 22.54.

XS
SM
MD
LG