Upatikanaji viungo

Breaking News
Ijumaa, Machi 29, 2024 Local time: 16:25

Magufuli awapa fursa ya mwisho wananuzi wa korosho


Rais John Pombe Magufuli
Rais John Pombe Magufuli

Rais Magufuli ametangaza Jumamosi iwapo wanunuzi binafsi hawatatii maagizo ya Serikali ya kununua korosho kwa bei isiyopungua shilingi 3,000 hawataweza kushiriki katika manunuzi hayo ifikapo Jumatatu saa nne asubuhi.

Kauli hiyo imekuja baada ya agizo lililotolewa Ijumaa na Waziri Mkuu Kassim Majaliwa.

Aidha serikali itachukua hatua ya kutumia Jeshi la Wananchi wa Tanzania (JWTZ) na Bodi ya Mazao mchanganyiko kununua korosho kwa bei ya zaidi ya shilingi 3,000 kwa kilo na hakutakuwapo mnunuzi yeyote binafsi atakaye shiriki katika ununuzi huo baada ya muda uliotolewa na serikali kumalizika.

Rais Magufuli amefafanua kuwa serikali pia itaangalia uwezekano wa kupatikana soko na korosho nyingine zitabanguliwa kwa ajili ya soko la ndani na nje ya nchi.

Serikali ya Tanzania imechukuwa hatua hiyo baada ya madai yaliyo andikwa katika vyombo vya habari nchini Tanzania kuwa wanunuzi binafsi wamegoma kununua korosho.

Vyombo vya habari vimeeleza kuwa serikali iliungana na msimamo wa wakulima wa korosho wa kukataa bei ya kati ya shilingi 1,900 hadi 2,700 kwa kilo, na hivyo kukubaliana kuwa korosho zitanunuliwa kwa bei isiyopungua shilingi 3,000 kwa kilo.

Kufikia Jumamosi kati ya kampuni 37 zilizoomba kununua korosho ni kampuni 14 tu ndizo zimejitokeza na ununuzi unafanyika polepole mno.

XS
SM
MD
LG