Upatikanaji viungo

Breaking News
Alhamisi, Aprili 25, 2024 Local time: 22:29

Maaskofu wa Kanisa Katoliki na wanasheria waikosoa serikali ya Zimbabwe


Raia wa Zimbabwe wakiandamana nje ya Ubalozi wa Zimbabwe mjini London kupinga kukithiri kwa ufisadi nchini Zimbabwe.
Raia wa Zimbabwe wakiandamana nje ya Ubalozi wa Zimbabwe mjini London kupinga kukithiri kwa ufisadi nchini Zimbabwe.

Maaskofu wa Kanisa Katoliki na chama cha wanasheria nchini Zimbabwe wameikosoa serikali kwa tuhuma za ukiukwaji wa haki za binadamu na ukamataji wa wapinzani, huku wasi wasi ukiongezeka juu ya namna serikali inavyowatendea wapinzani na mzozo mbaya wa kiuchumi.

Rais Emmerson Mnangagwa amejibu kwa haraka sana, akisema tuhuma hizo mbaya zinazoelezewa hazina msingi wowote.

Mfumuko wa bei umeongezeka kwa zaidi ya asilimia 800, ikiwa ni dhahiri kwamba Zimbabwe inakabiliwa na mzozo mbaya wa kiuchumi katika kipindi cha muongo mmoja.

Hali hii imefufua kumbukumbu za mfumuko mbaya sana wa bei chini ya utawala wa miaka 37 wa hayati Rais Robert Mugabe, utawala uliomalizwa na mapinduzi ya kijeshi mwaka 2017.

Maaskofu walisema katika barua yao kwamba taifa linakabiliwa na mfululizo wa mizozo, ikiwemo uchumi unaodorora, umaskini uliokithiri, rushwa na ukiukwaji wa haki za binadamu.

Akijibu barua hiyo ya maaskofu wa Kanisa Katoliki, waziri wa habari Monica Mutsvangwa amemkosoa kiongozi wa mkutano wa maaskofu katoliki Robert Ndlovu, na kuielezea barua ya maaskofu hao kama ujumbe wa kishetani, wenye lengo la kuchochea mauaji wa halaiki kama yaliotokea nchini Rwanda.

Wakosoaji wanamshtumu Mnangagwa, ambaye alikuwa makamu rais wa Robert Mugabe, kwa kutumia mifumo ya kidikteta kama ile iliyoshuhudiwa wakati wa utawala wa mtangulizi wake.

XS
SM
MD
LG