Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumapili, Mei 05, 2024 Local time: 17:11

Waandamanaji Zimbabwe wamepanga maandamano mengine leo


Waandamanaji huko Zimbabwe wakizuiwa na polisi kuandamana dhidi ya serikali ya Rais Mnangagwa
Waandamanaji huko Zimbabwe wakizuiwa na polisi kuandamana dhidi ya serikali ya Rais Mnangagwa

Hatua hii inafuata licha ya ukamataji uliofanyika Jumatatu saa kadhaa kabla ya maandamano kuanza ambayo yalipigwa marufuku na polisi wa Zimbabwe na hatimaye waziri wa mambo ya nje na biashara ya kimataifa kutetea hatua iliyochukuliwa na vyombo vya dola

Waziri wa mambo ya nje na biashara ya kimataifa nchini Zimbabwe, Sibusiso B. Moyo ameutetea ukamataji uliofanyika Jumatatu kwa waandamanaji wanaoipinga serikali na alitoa wito kuwepo hali ya kustahmiliana katika kipindi hiki cha kurejesha uchumi wa nchi hiyo ulioharibika.

Moyo aliiambia Sauti ya Amerika-VOA wakati wa mahojiano kwamba japokuwa kila mtu ana haki ya kuandamana, kumekuwepo na kampeni nyingi zinazochochea ghasia na kukiuka usalama wa umma. Alikubaliana na mahakama ya Zimbabwe kuunga mkono marufuku iliyokwekwa na polisi kwa maandamano yaliyoandaliwa na ushirika wa upinzani wa Movement for Democratic Change-MDC.

Rais wa Zimbabwe, Emmerson Mnangagwa
Rais wa Zimbabwe, Emmerson Mnangagwa

Viongozi wa ushirika wanamshinikiza Rais Emmerson Mnangagwa na chama chake tawala cha ZANU-PF kusimamia jukumu la serikali ya mseto. Maandamano mengine yamepangwa kufanyika Jumanne kati kati ya mji wa Gweru na mengine Jumatano huko kusini mashariki mwa mji wa Masvingo nchini Zimbabwe.

Awali viongozi hao walipanga maandamano ambayo yalipigwa marufuku Jumatatu na maafisa polisi huko Bulawayo, mji wa pili kwa ukubwa nchini Zimbabwe

XS
SM
MD
LG