Maandamano ya #EndSARS yaliyoongozwa na vijana yalikuwa makubwa kuliko yote dhidi ya serikali katika historia ya sasa ya Nigeria, lakini yalimalizika kwa ukandamizaji uliofanywa na majeshi ya usalama na mizozo mikali kama iwapo baadhi yao walipigwa risasi na wanajeshi.
Serikali ya jimbo la Lagos na vikosi vya jeshi kila mara vimekuwa vikikanusha kuwa wanajeshi walifyatua risasi, kulenga eneo la Lekki lilipo lango eneo la kulipia ushuru katika jiji la Lagos, ambalo ndiyo kitovu cha maandamano hayo, lakini jopo huru liliamua kuwa katika "mauaji" hayo, waandamanaji hawakuwa na silaha.
Shirika la kutetea haki za binadamu la Amnesty linasema takriban watu 10 waliuawa kwa kupigwa risasi na vikosi vya usalama mnamo tarehe 20 Oktoba mwaka 2020 kwenye lango la kulipia ushuru, na wengine waliuawa katika fujo na ghasia zilizozuka sehemu nyingine za jiji la jimbo hilo la Lagos.
Katika taarifa ya Jumapili jioni, wizara ya afya ya jimbo la Lagos ilisema waathirika 103 ambao miili yao imewekwa katika vyumba vya kuhifadhia maiti mjini Lagos kwa muda wa miaka mitatu bado haijadaiwa na familia, kwa hiyo itazikwa kwa pamoja hivi karibuni.
Ilisema miili iliokotwa kutoka maeneo kadhaa kuzunguka jimbo la Lagos, lakini ilikanusha kuwa ilikusanywa kutoka eneo la Lekki, baada ya nakala ya mpango wa mazishi kuvuja kwenye vyombo vya habari vya ndani ya nchi hiyo.
Ni mara ya kwanza kwa taarifa ya wizara ya afya kukiri kuwa serikali imekubali kuwa na idadi kubwa ya watu walifariki kufuatia ghasia hizo.
Chanzo cha habari hii nia shirika la habari la AFP
Forum