Kiwango cha wastani cha matumizi ya kila siku ya petroli yameshuka hadi kufikia lita milioni 48.43 lita kwa mwezi Juni, kutoka kiwango cha awali cha wastani wa lita milioni 66.9 , kulingana na takwimu zilizotolewa na Mamlaka ya ya kusimamia petroli Nigeria (NMDPRA).
Ruzuku iliifanya bei ya petrol kubaki kuwa nafuu kwa miongo kadhaa katika nchi hiyo yenye uchumi mkubwa barani Afrika, lakini gharama zilizidi kuwa kubwa kwa nchi – serikali ilitumia dola bilioni kumi mwaka jana – na kusababisha upungufu mkubwa wa fedha na kuifanya serikali kutumbukia katika madeni.
Tangu ruzuku ilipositishwa, soko la biashara ya magendo katika nchi jirani za Cameroon, Benin na Togo, ambazo zilikuwa zikitegemea mafuta ya magendo kutoka Nigeria limeporomoka.
Benki ya Dunia ilisema tarehe 27 Juni, kwamba licha ya kutumia dola bilioni 2.41 kwa ruzuku hiyo miezi mitano ya kwanza, Nigeria imeweza kuokoa hadi dola billioni 5.10 mwaka huu kutokana na kuondolewa ruzuku kwenye petroli na kufanya mageuzi kwenye soko lake la kubadilisha fedha za kigeni.
Mara ya mwisho serikali ilipojaribu kuondoa ruzuku hiyo mwaka 2012, ilisababisha maandamano nchi nzima. Tinubu, ambaye wakati huo alikuwa kiongozi wa upinzani, alipinga kuondolewa kwa ruzuku hiyo.
Chanzo cha habari hii ni shirika la habari la Reuters
Forum