Saudi Arabia imesema itapunguza uzalishaji wa mafuta kwa mapipa milioni moja kwa siku kwa kipindi cha mwezi mmoja mwingine ukiwemo mwezi wa Agosti, ikiongeza kuwa hatua ya kupunguza uzalishaji wa mafuta itaendelea baada ya Agosti.
Muda mfupi baada ya tangazo hilo la Saudi Arabia, naibu waziri mkuu wa Russia Alexander Novak amesema Moscow itapunguza mauzo ya nje ya mafuta yake kwa mapipa 500,000 kwa siku mwezi Agosti.
Kiwango kilichopunguzwa na nchi hizo mbili ni sawa na asilimia 1.5 ya mafuta yanayouzwa duniani na kufikia kiwango cha hadi mapipa milioni 5.16 kwa siku ambacho nchi zinazozalisha mafuta wanachama wa OPEC zilikuwa zimeahidi kupunguza.
Baada ya taarifa ya kupunguzwa kwa uzalishaji wa mafuta, bei ya mafuta ghafi kwenye soko la kimataifa imeongezeka kwa senti 89 hadi dola 76.30 kwa pipa moja.
Forum