Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumapili, Machi 23, 2025 Local time: 22:53

Lori la mafuta lalipuka Nigeria na kuua watu nane


Mabaki ya lori la mafuta lililoshika moto baada ya kupata ajali huko Lokoja, Nigeria, Septemba 23, 2020. Picha na Haruna Yahaya / AFP.
Mabaki ya lori la mafuta lililoshika moto baada ya kupata ajali huko Lokoja, Nigeria, Septemba 23, 2020. Picha na Haruna Yahaya / AFP.

Takriban watu nane waliuawa wakati lori la mafuta lilipolipuka huko kusini magharibi mwa Nigeria, ajali hiyo imetokea wakati wakaazi wa eneo hilo walipokuwa wakijaribu kuchota petroli iliyokuwemo katika lori hilo, polisi walisema Jumatatu.

Ajali hiyo iliyotokea Jumapili usiku katika kitongoji cha Ondo, wakati lori hilo lilipopinduka baada ya kuserereka na kuacha barabara, polisi walisema.

"Baadhi ya watu walikwenda katika eneo la ajali na kuchota mafuta, wakati wa tukio hilo gari la mafuta lilipuka," msemaji wa polisi wa jimbo la Ondo, Fumilayo Odunlami-Omisanya alisema.

Bei ya petroli imeongezeka nchini Nigeria kwa zaidi ya mara tatu tangu kuondolewa kw a ruzuku iliyokuwepo kwa miongo kadhaa mwishoni mwezi Mei, na kuwathiri madereva na kaya pamoja na wafanyabiashara wadogo wadogo ambao wana majenereta yanayotumia petroli.

Chanzo cha habari hii ni Shirika la habari la Reuters

Forum

XS
SM
MD
LG