Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumatano, Januari 22, 2025 Local time: 14:57

Kanisa Lagos linavyokabiliana na unyanyapaaji wa walemavu


Watu wenye ulemavu wa macho wakiimba wakati wa ibada ya Jumapili katika kanisa la Bethesda Home huko Lagos, Nigeria Julai 2, 2023. Picha na REUTERS/Seun Sanni.
Watu wenye ulemavu wa macho wakiimba wakati wa ibada ya Jumapili katika kanisa la Bethesda Home huko Lagos, Nigeria Julai 2, 2023. Picha na REUTERS/Seun Sanni.

Kila Jumapili, waumini wa Kanisa la Bethesda Home mjini Lagos wamekuwa wakiimba na kucheza nyimbo maarufu. Lakini kuna kitu ambacho si cha kawaida: wapiga ngoma, gitaa, wapiga kibodi (keyboard)na kwaya nzima wana ulemavu wa kutoona.

Ingawa mitazamo inabadilika, nchini Nigeria takriban watu milioni 25 wanaoishi na ulemavu bado wanakabiliwa na unyanyapaa pamoja na ubaguzi kutokana na dhana potofu kuhusu sababu za ulemavu, kulingana na Benki ya Dunia.

Kutokana na kuchoshwa kuona vipofu wanatengwa kijamii makanisani, Chioma Ohakwe alianzisha Kanisa la Bethesda Home miaka mitatu iliyopita, ili kuwakuza na kusherehekea vipaji vya wanamuziki, pamoja na kuandaa mahali pa ibada kwa waumini ambao wengi wao wana matatizo ya kuona.

"Wakati (watu) watakapoanza kuona uwezo wao, watawaaminini,” alisema Ohakwe, ambaye anaendesha shirika lisilo la kiserikali kwa wasio na uwezo wa kuona.

Wakiwa wamevaa mashati meupe na tai zinazofanana za rangi nyekundu, bendi huwaamsha waumini waliohudhuria kwa milio yenye hisia ya kufurahisha kwa sauti na vishindo.

Katika safu ya mbele ya kwaya husimama Nathaniel Ndukwe, "Mr. Blind Nigeria 2023", akiwa na mtindo wa nywele zenye rangi ya blond na viatu vya dhahabu vinavyometa.

"Ingawa uwezo wa kuona haupo, maono yetu bado ni makubwa sana,” alisema.

"Nataka kila mtu popote alipo, nikiwa kama kipofu au mtu mlemavu, aelewe kuwa kuna mengi bado unaweza kufanya ikiwa unajiamini."

Mwimbaji mwingine, Ogungbe Abiola, alisema anataka muziki wao kusaidia kushinda mioyo na mawazo, katika nchi hiyo ambayo, kulingana na Benki ya Dunia, viwango vya ukosefu wa ajira miongoni mwa watu wenye ulemavu ni karibu mara mbili ya jumla ya idadi ya watu.

"Tunaweza kuuonyesha ulimwengu kwamba ndiyo, kuna uwezo wa kweli ndani ya ulemavu," Abiola alisema.

Chanzo cha habari hii Shirika la habari la Reuters

Forum

XS
SM
MD
LG