Upatikanaji viungo

Breaking News
Alhamisi, Septemba 19, 2024 Local time: 12:46

Kipindupindu kutishia Malawi


Watoto wawili wa kiume, mmoja wakivua samaki katika mto Mtandile mjini Lilongwe, Februari 20, 2023. Eneo ambalo limeathirika sana na mlipuko wa ugonjwa wa kipindupindu kutokana na uhaba wa maji safi ya kunywa. Picha na Fredrik Lerneryd / AFP.
Watoto wawili wa kiume, mmoja wakivua samaki katika mto Mtandile mjini Lilongwe, Februari 20, 2023. Eneo ambalo limeathirika sana na mlipuko wa ugonjwa wa kipindupindu kutokana na uhaba wa maji safi ya kunywa. Picha na Fredrik Lerneryd / AFP.

Malawi inakabiliwa na hatari ya ongezeko la wagonjwa wa kipindupindu kufuatia uharibifu uliosababishwa na kimbunga Freddy ambacho kimeharibu mifumo ya maji na vyoo, wizara ya afya ilionya Jumatatu.

Nchi hiyo ambayo ilikuwa tayari ikipambana mlipuko mkubwa wa kipindupindu ambao haujawahi kurekodiwa wakati dhoruba ya kimbunga Freddy ilipotua wiki iliyopita, na kusababisha maporomoko ya matope na mafuriko, ambapo watu 476 walipoteza maisha na wengine takribani nusu milioni kukoseshwa makazi.

Mlipuko wa kipindupindu nchini humo uliozuka mwaka jana, ambapo watu zaidi ya 30,600 waliambukizwa na wengine zaidi ya 1,700 kupoteza maisha.

"Mafuriko yamesomba vyoo na kusababisha idadi kubwa ya watu kukosa maji safi ya kunywa," mkurugenzi wa huduma za afya, Storn Kabuluzi aliliambia shirika la habari la AFP, na kusema nchi hiyo "iko hatarini" kutokana na ongezeko la visa vya wagonjwa wa kipindupindu.

Baada ya mashambulizi ya kimbunga hicho kilichovunja rekodi, dhoruba hiyo ilisababisha vifo vya watu 579 katika nchi tatu za kusini mwa Afrika zikiwemo Msumbiji na Madagascar.

Malawi ni nchi iliyoathirika zaidi wakati kimpunga Freddy kiliposababisha mafuriko na maporomoko ya udongo ambayo yalisomba nyumba, barabara na madaraja – na kusababisha uharibifu mkubwa wa miundo mbinu ya maji nchini humo.

Katika nchi jirani ya Msumbiji, kusitishwa kwa huduma za maji, afya na usafi wa mazingira "kunasababisha kasi ya ongezeko la wagonjwa wa kipindupindu", lilisema Shirika la Umoja wa Mataifa la kuhudumia Watoto (UNICEF) kanda ya Mashariki na Kusini mwa Afrika.

Chanzo Cha bahari hii ni shirika la habari la AFP.

XS
SM
MD
LG