Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumapili, Juni 23, 2024 Local time: 08:38

Kimbunga Freddy chaua watu 190 Malawi


Barabara inayo iunganisha miji ya Blantyre na Lilongwe ikiwa imeharibiwa na mvua kubwa iliyosababishwa na Kimbunga Freddy huko Blantyre, Malawi, Machi 14 2023. Picha na Shirika la habari la AP /Thoko Chikondi.
Barabara inayo iunganisha miji ya Blantyre na Lilongwe ikiwa imeharibiwa na mvua kubwa iliyosababishwa na Kimbunga Freddy huko Blantyre, Malawi, Machi 14 2023. Picha na Shirika la habari la AP /Thoko Chikondi.

Idadi ya vifo nchini Malawi vilivyo tokana na Kimbunga Freddy imeongezeka maradufu na kufikia watu 190 Jumanne.

Baada ya dhoruba hiyo iliyovunja rekodi kusababisha mafuriko na maporomoko ya ardhi wakati kimbunga hicho kilipopiga kwa mara ya pili eneo hilo la kusini mwa Afrika katika kipindi cha chini ya wiki tatu.

Baada ya kusababisha maafa nchini Australia mapemwa mwezi Februari, Freddy kilivuka Bahari ya Hindi, na kutua Kusini Mashariki mwa Afrika mwishoni mwa mwezi Februari. Mwishoni mwa wiki iliyopita kimbunga hicho kilirejea eneo hilo na kupiga kwa mara ya pili.

"Idadi ya watu waliofariki imeongezeka kutoka watu 99... hadi 190, huku watu 584 wakiwa wajeruhiwa na 37 wameripotiwa kutojulikana walipo," Idara ya Masuala ya Kukabiliana na Majanga nchini Malawi ilisema katika taarifa yake.

Wafanyakazi wanaotoa misaada walisema idadi ya vifo inatarajiwa kuongezeka.

"Hali ni mbaya sana," alisema Guilherme Botelho, mratibu wa mradi wa dharura wa shirika la kujitolea la Madaktari Wasio na Mipaka (MSF).

"Kuna majeruhi wengi, waliojeruhiwa, waliopotea au kufariki, na idadi hii inatarajiwa kuongezeka katika siku zijazo."

Watu wengi wameangamia kutokana na maporomoko ya matope yaliyozisomba nyumba katika mji mkuu wa kibiashara wa Blantyre.

Wengi wanaamini kuwa kuna watu bado wamekwama chini ya vifusi vya matope -- lakini hakuna waokoaji.

Takribani watu 59,000 wameathiriwa, na zaidi ya 19,000 wamekoseshwa makazi.

Chanzo cha habari hii ni shirika la habari la AFP.

XS
SM
MD
LG