Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumapili, Septemba 15, 2024 Local time: 00:56

Umoja wa Mataifa wataka misaada zaidi kukabiliana na Kipindupindu, Malawi


Umoja wa  Mataifa nchini Malawi umezindua ombi la haraka  la  msaada wa  kukabiliana na mlipuko ulioweka rekodi ya kipindupindu ambao mpaka sasa umesababisha vifo vya watu 1,450, na kuambukiza 45,000.

Wataalamu wa afya nchini humo wanasema kama hatua za haraka hazita chukuliwa kuongeza juhudi za kukabiliana na hali hiyo, idadi ya maambukizi inaweza kuongezeka mara mbili katika miezi michache ijayo.

Umoja wa Mataifa unasema mwito huo wa haraka unahitaji kukusanya dola milioni 45.3 ili kutoa msaada wa kuokoa maelfu ya watu wa Malawi walio taabika na kipindupindu.

Katika taarifa iliyotolewa Jumatatu, Umoja wa Mataifa unasema mwito huo una malengo ya kuwasaidia watu milioni 4 nchini Malawi, ikijumuisha wakimbizi 56,000 na wanaotafuta hifadhi ambao wapo katika hatari ya mlipuko huo.

Mlipuko wa sasa wa kipindupindu ulianza Machi mwaka jana, na umesambaa katika wilaya zote 29 za Malawi. Rebecca Adda-Dontoh, ni mwakilishi mkazi wa Umoja wa Mataifa nchini Malawi.

Amewaeleza wanahabari kwamba msaada zaidi unahitajika kuzuia mlipuko.

“Kazi kubwa imefanyika, lakini zaidi inahitajikan kufanyika. Tumejikita katika afya na zaidi katika usafi na maji kiujumla. Hayo mawili ni muhimu sana lakini pia sekta nyingine za liche, kinga, na pia uratibu kwa sababu tunahitaji kusambaza kutoka sehemu moja kwenda nyingine.”

Adda-Dontoh amesema msaada unao hitajika utawasaidia wadau wengine wa ufadhili ambao tayari wamesha changia.

“Umoja wa mataifa pekee umesha kusanya karibu dola milioni 10. Umesikia EU,imechangia Euro 500,00 na UK paundi 500,000. Hata serekali ya Malawi ipo inafanyakazi na tayari imechangia.”

Vyombo vya habari nchini humo vimeripoti kwamba Malawi inahitaji dola milioni 40 za ziada kwa mpango wake wa kitaifa wa kukabiliana na kipindupindu.

Maambukizi ya kipindupindu yameongeneka Malawi toka kuanza kwa Januari na kuwa mabaya kama mlipuko mkubwa zaidi katika miongo miwili iliyopita.

Rais wa Malawi, Lazarus Chakwera, amesema wiki iliyopita wakati akizundua kampeni ya kitaifa ya kukabiliana na kipindupindu, kwamba vituo vya afya vya malawi vilirekodi kati ya maambukizi ya kipindupindu 500 na 600 kila siku.

Umoja wa Mataifa umesema kwamba wataalamu wa afya walionya kwamba Malawi ingeweza kurekodi kati ya maambukizi ya kipindupindu zaidi ya 64,000 na 100,000 katika kipindi cha miezi mitatu ijayo labda hatua za haraka zichukuliwe kuongeza juhudi za kukabiliana na mlipuko.

XS
SM
MD
LG