Upatikanaji viungo

Breaking News
Alhamisi, Machi 28, 2024 Local time: 15:17

Kifo cha Shinzo Abe: Polisi wakiri kutokuwepo usalama wa kutosha wakati wa shambulizi


PICHA YA MAKTABA: Mshukiwa wa shambulizi lililopelekea kifo cha waziri mkuu wa zamani wa Japan Shinzo Abe akidhibitiwa na maafisa wa usalama mjini Nara muda mfupi baada ya shambulio hilo. Baadaye alipelekwa kwa kituo cha polisi cha Saidaiji, mjini Nara.
PICHA YA MAKTABA: Mshukiwa wa shambulizi lililopelekea kifo cha waziri mkuu wa zamani wa Japan Shinzo Abe akidhibitiwa na maafisa wa usalama mjini Nara muda mfupi baada ya shambulio hilo. Baadaye alipelekwa kwa kituo cha polisi cha Saidaiji, mjini Nara.

Msafara uliousindikiza mwili wa Waziri Mkuu wa zamani wa Japan Shinzo Abe uliwasili Jumamosi nyumbani kwake katika mji mkuu wa nchi hiyo, Tokyo, huku polisi katika mji wa magharibi wa Nara ambako aliuawa wakikiri kwamba hakukuwa na usalama wa kutosha wakati wa tukio hilo.

Waombolezaji walikusanyika katika makazi yake na katika eneo la shambulio la Ijumaa huko Nara, ambapo kiongozi huyo aliyekaa madarakani kwa muda mrefu, katika historia ya karibuni ya Japan, aliuawa kwa kupigwa risasi katika tukio nadra la vurugu za kisiasa alipokuwa akihutubia mkutano wa kampeni.

Viongozi wa kisisa nchini humo wamesema mauaji hayo ni shambulizi dhidi ya mfumo wa demokrasia. Polisi walimkamata mwanamume mwenye umri wa miaka 41 mara baada ya Abe kupigwa risasi kwa karibu, na walisema mshukiwa alitumia bunduki ya kujitengenezea.

Jeshi la polisi la eneo hilo lililosimamia hafla ya kampeni lilisema Jumamosi kwamba mipango ya usalama ilikuwa na kasoro. "Hatuwezi kukataa kwamba kulikuwa na matatizo katika mpango wa usalama kutokana na jinsi mambo yalivyomalizika," mkuu wa polisi wa eneo la Nara Tomoaki Onizuka aliambia mkutano wa wanahabari.

"Ninahisi hisia kubwa ya kuwajibika," alisema, akiongeza kuwa polisi watachunguza tukio hilo na kutekeleza mabadiliko yoyote muhimu. Uchaguzi wa viti katika baraza la juu la bunge la Japan utaendelea kama ulivyopangwa Jumapili.

Waziri Mkuu Fumio Kishida alirejea kwenye kampeni akitembelea maeneo bunge kadhaa baada ya kurejea Tokyo kwa dharura siku ya Ijumaa baada ya shambulizi hilo.

XS
SM
MD
LG