Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumanne, Mei 28, 2024 Local time: 04:49

Waziri mkuu wa zamani wa Japan, Shinzo Abe, auwawa

Picha iliyotolewa kwenye video, waziri mkuu wa zamani Shinzo Abe, akiwa katika mkutano wa kampeni mjini Nara, magharibi mwa Japan kabla hajapigwa risasi Ijumaa, Julai 8, 2022. Alifyatuliwa risasi wakati akitoa hotuba, na alikimbizwa hospitali na helkopta lakini akiwa hapumuwi.

Shinzo Abe, waziri mkuu wa zamani wa Japan ambaye alikuwa na ushawishi, amefariki dunia baada ya kupigwa risasi kifuani wakati akitoa hotuba leo, kwa mujibu wa maafisa wa Japan.

Mapema Ijumaa, Abe alikuwa akizungumza katika tukio la kampeni nje ya kituo cha treni cha mji wa Nara, mashariki mwa Osaka, ambapo mtu mwenye bunduki alikwenda nyuma yake.

Kufuatia milio miwili mikubwa, Abe alidondoka chini huku akitokwa damu.

Video zilizotolewa katika mitandao ya kijamii zilionyesha watu wakikusanyika kumpatia msaada Abe, ambaye alikuwa amelala chini bila kufanya chochote.

Abe mwenye umri wa miaka 67 alipelekwa hospitali ambapo mitandao ya kijamii ilisema kwamba alipatwa na mshtuko wa moyo.

Shirika la utangazaji la Japan NHK limesema aliyehusika na tuki hilo ni mwanaume mwenye umri wa miaka 41 kutokea Nara na ameshikiliwa na vyombo vya usalama.

XS
SM
MD
LG