Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumanne, Septemba 10, 2024 Local time: 21:28

Kesi dhidi ya Trump ya madai kuzuia uchunguzi yapamba moto


Rais Donald Trump akiongea na waandishi wa habari White House Octoba 11, 2019.
Rais Donald Trump akiongea na waandishi wa habari White House Octoba 11, 2019.

Kesi dhidi ya utawala wa Trump ya madai ya kuzuia uchunguzi inazidi kupamba moto, kama Mwakilishi wa chama cha Democrat Adam Schiff alivyosema.

Kuongezeka kasi kwa kesi hiyo anasema inatokana na wanachama wa ngazi ya juu na mwanasheria wa Trump binafsi, Rudy Giuliani kupuuza hati ya wito juu ya shauri la uchunguzi linalotaka kumuondoa madarakani rais.

Ofisi ya makamu wa rais Mike Pence imeuita uchunguzi wa baraza la wawakilishi linalongozwa na wa Democrat, ni utashi wao wenyewe na hati ya kuitwa kujibu maswali ni pana mno.

Wizara ya Ulinzi ya Marekani,Pentagon, pia imesema haina uwezo kutoa ushirikiano kwa muda huu kutokana na sababu za kisheria.

Ofisi ya bajeti ya White House pia imekataa ombi la Baraza hilo, na mwanasheria binafsi wa Rais Trump, Rudy Giuliani pia amekataa kuitika wito wa hati inayomtaka kutoa nyaraka zinazohusiana na juhudi za kuishinikiza Ukraine kumchunguza makamu wa rais wa zamani na mgombea urais wa Democrat hivi sasa, Joe Biden.
Jioni Jumanne, Mwakilishi wa Baraza la Wawakilishi Michael McCaul, kiongozi wa Republikan katika Kamati ya Mambo ya Nje, amesema uchunguzi wa kumuondoa rais madarakani "unaoendelea kwa faragha ambapo ilitakiwa ufanyike hadharani."

"Namtaka Spika aweke azimio hilo hadharani ili tuendelee katika njia ya uwazi na suala hili hali ya kuwa watu wote wa Marekani wanafahamu kile kinachoendelea kwa sababu mwisho wa siku, ni wao ambao wataathirika na mchakato usiokuwa wa haki," McCaul amesema.

Lakini Schiff amesema Warepublikan wamewakilishwa ipasavyo katika mahojiano hayo ya faragha, akisema wanapewa kila fursa kuwahoji mashahidi na kuona ushahidi.

Those hearings continue Wednesday with testimony from Michael McKinley, a former senior advisor to Secretary of State Mike Pompeo.

Mahojiano hayo yanaendelea siku ya Jumatano ambapo Michael McKinley atatoa ushahidi, yeye ni mshauri wa ngazi ya juu wa Waziri wa Mambo ya Nje Mike Pompeo.

XS
SM
MD
LG