Upatikanaji viungo

Breaking News
Alhamisi, Desemba 05, 2024 Local time: 22:54

Balozi Yovanovitch kutoa ushahidi katika kesi ya Trump


Balozi Marie Yovanovitch
Balozi Marie Yovanovitch

Balozi wa zamani wa Marekani nchini Ukraine, Marie Yovanovitch amepangiwa kutoa ushahidi mbele ya kamati ya bunge inayoongoza uchunguzi wa kufunguliwa mashtaka ya kuondolewa mamlakani Rais Donald Trump.

Hata hivyo haiko wazi iwapo kamati hiyo itaweza kusonga mbele na mkutano wao wa Ijumaa atakao hudhuria Yovanovitch.

White House inakataa kushirikiana na bunge katika uchunguzi wa kufunguliwa mashtaka ya kuondolewa mamlakani ikidai kuwa unakiuka katiba.

Na Wizara ya Mambo ya Nje ya Marekani, imemzuia balozi wa Marekani katika Umoja wa ulaya na mfadhili wa Trump, Gordon Sondland kutoa ushahidi kwa hiari yake.

Rais Trump anaendelea kusema kwamba mazungumzo yake ya simu ya Julai 25 na Rais wa Ukraine Volodymyr Zelensky, ambayo yamechochea uchunguzi wa Trump na kufunguliwa mashtaka hayakuwa kinyume na sheria.

Imetayarishwa na mwandishi wetu, Washington, DC.

XS
SM
MD
LG