Mapema mwaka 2021, Kenya ilipiga marufuku uagizaji wa bidhaa hizo ikiwemo kuku na mayai kutoka Afrika Mashariki ikisema kuwa inahitaji kulinda na kuwaunga mkono wazalishaji wake kurejea katika hali ya kawaida baada ya janga la COVID-19 kuharibu uzalishaji.
Kenya imekuwa juu katika bidhaa hizo, pia ilipiga marufuku nyama, maziwa na mahindi kutoka Uganda na kumzuia jirani yake upande wa magharibi kupoteza mabilioni ya dola ya fedha za kigeni.
Mapema mwezi Disemba, Baraza la Mawaziri lilipitisha hatua ambayo iliifanya Uganda kujibu kwa kuweka marufuku kwenye bidhaa za Kenya.
Hata hivyo Jumanne serikali zote mbili zilifanya mazungumzo ya kibiashara mjini Nairobi.
Baada ya mkutano huo wa pamoja ilikubaliwa kwa ajili ya manufaa ya nchi zote mbili masharti yaliyowekwa yaondolewe.
Mkutano huo unafuatia ukosoaji mkubwa uliofanywa na wazalishaji wa bidhaa hizo ambapo waliishutumu Wizara ya Kilimo kwa kutowasaidia kuondokana na marufuku iliyowekwa na serikali ya kenya .