Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumamosi, Julai 20, 2024 Local time: 15:52

Kasisi asema Wayahudi hawatakatishwa tamaa na shambulizi la Sinagogi


Kasisi Yisroel Goldstein, kulia, akifarijiwa na waumini wakati akiondoka kutoka katika mkutano wa waandishi wa habari huko Chabad, katika Sinagogi la Poway Jumapili, Aprili 28, 2019
Kasisi Yisroel Goldstein, kulia, akifarijiwa na waumini wakati akiondoka kutoka katika mkutano wa waandishi wa habari huko Chabad, katika Sinagogi la Poway Jumapili, Aprili 28, 2019

Mmoja wa manusura wa shambulizi la risasi katika sinagogi ya Chabad karibu na San Diego, Kasisi Yisroel Goldstein, Jumapili ameeleza jinsi alivyopoteza kidole kwa kupigwa risasi na kusisitiza kuwa hilo halitawakatisha tamaa kuendelea na ibada.

Kasisi huyo amewataka Wayahudi wote kwenda katika sinagogi zao Ijumaa hii usiku, ambapo inaanza ibada ya Sabato ya Wayahudi, kuonyesha umoja wao na "kuwa ugaidi hauwezi kufanikiwa."

"Sisi ni taifa la Kiyahudi ambalo litaendelea kuwa juu. Hatutaruhusu mtu yoyote au kitu chochote kutukandamiza. Lazima tupambane na kiza kwa kutumia muangaza," amesema.

Mshauri wa usalama wa taifa John Bolton amesema "hakuna shaka" shambulizi la bunduki ndani ya sinagogi Jumamosi mjini San Diego lilikuwa ni jinai ya chuki, lakini kunauwezekano kuwa mtu huyo anayetuhumiwa kuua na kujeruhi alikuwa peke yake.

"Ilikuwa ni kitendo cha kinyama na ni kitendo kisichoweza kutafutiwa udhuru wowote," Bolton aliliambia shirika la habari la Fox News Jumapili.

Amesimulia kwa waandishi wa habari kuwa licha ya kujisalimisha na kuinua mikono hewani akimwomba mshambulizi asimpige risasi, mtu huyo aliendelea kumrushia risasi.

Jumamosi mzungu mmoja aliyekuwa amejihami kwa bunduki alivamia sinagogi hiyo na kumuua mwanamke mmoja na kujeruhi waumini wengine wawili wakati maombi yakiendelea.

Taarifa ya White House inasema kwamba Rais Donald Trump amesisitiza upendo wake kwa jamii ya Wayahudi na jamii nzima ya Poway, katika mazungumzo ya simu ya dakika 15 na mmoja wa manusura hao.

Imetayarishwa na mwandishi wetu, Washington, DC.

XS
SM
MD
LG