Upatikanaji viungo

Breaking News
Ijumaa, Januari 24, 2025 Local time: 02:50

Kamati ya bunge Libya yatangaza kuahirisha uchaguzi wa rais Ijumaa


Mtu akijiandikisha kupiga kura huko Libya katika kituo cha kupiga kura Tripoli, Novemba 8, 2021, Libya. (Photo by Mahmud TURKIA / AFP)
Mtu akijiandikisha kupiga kura huko Libya katika kituo cha kupiga kura Tripoli, Novemba 8, 2021, Libya. (Photo by Mahmud TURKIA / AFP)

Kamati ya bunge la Libya ilisema Jumatano haitaweza kufanya uchaguzi wa rais siku ya Ijumaa.

Mwenyekiti wa kamati alitoa tathmini yake katika barua kwa mkuu wa bunge akisema ilikuja baada ya mashauriano kwa ripoti za kiufundi, mahakama na usalama. Mwenyekiti hakutaja tarehe mpya itakayofanyika uchaguzi huo.

Mizozo mingi kuhusu mchakato wa uchaguzi iliibua matarajio kwamba upigaji kura uliosubiriwa kwa muda mrefu huenda ungecheleweshwa. Libya inafanya kazi chini ya serikali ya mpito kwa miaka 10 baada ya kuondolewa madarakani kwa kiongozi wa muda mrefu Moammar Ghadhafi na pande zinazohasimiana katika eneo la mashariki na magharibi mwa nchi hiyo ziliingia katika sitisho la mapigano kwa mwaka uliopita chini ya mchakato wa Amani unaoungwa mkono na Umoja wa Mataifa.

Jana Jumanne tume ya Umoja wa mataifa nchini Libya ilielezea wasi wasi wake kuhusu hali ya usalama mjini Tripoli ambapo ilisema kukusanyika kwa vikosi vinavyoshirikiana na makundi mbali-mbali kunazua hali ya wasi wasi na kuongeza hatari ya mapigano ambayo yanaweza kuzusha mgogoro.

XS
SM
MD
LG