Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumatatu, Mei 06, 2024 Local time: 04:25

Gaddafi, Haftar wapata pigo katika kuwania urais Libya


Raia wa Libya
Raia wa Libya

Mwendesha mashtaka ya kijeshi nchini Libya Mohamed Gharouda, ameomba tume ya uchaguzi nchini humo kusitisha utaratibu wa kukubali jina la mwanawe aliyekuwa rais Muammar Gaddafi, Saif al-Islam Gaddafi, kuwa mgombea wa urais.

Ameomba pia kusitishwa kwa maombi ya kiongozi wa kundi la wapiganaji Khalifa Haftar, anaetaka kukombania urais.

Tume ya uchaguzi ilisema Jumapili kwamba Gaddafi alikuwa amewasilisha karatasi zinazohitajika kugombea urais katika uchaguzi wa mwezi ujao.

Katika barua kwa tume ya uchaguzi, Gharouda ameonya kwamba tume hiyo itawajibika kwa hatari itakayotokea endapo itaendelea na kuidhinisha majina ya wagombea hao.

Ofisi ya mkuu wa sheria imesema kwamba Saif al-Islam na Khalifa Haftar, wameshutumiwa kwa matendo ya uhalifu na kwamba azma yao ya kugombea urais inastahili kufutiliwa mbali.

Gaddafi anashutumiwa kwa ukiukwaji mkubwa wa haki za kibinadamu wakati wa utawala wa baba yake, ambao uliwalenga wapinzani.

Anatafutwa na mahakama ya kimataifa ya uhalifu kujibu mashtaka ya halifu wa kivita uliofanyika mwaka 2011..

Haftar, ambaye ana kikosi cha wapiganaji mashariki mwa Libya, anatafutwa na mahakama ya Marekani kwa kuwanyanyasa raia wa Libya.

XS
SM
MD
LG