Upatikanaji viungo

Breaking News
Ijumaa, Septemba 20, 2024 Local time: 04:26

Ferry ya kwanza kutoka Libya yaelekea Uturuki baada miaka 40


Ramani ya Misrata. Libya
Ramani ya Misrata. Libya

Ferry ya kwanza kutoka bandari ya Libya ya Misrata Jumatano imeng’oa nanga kuelekea  kwenye mji wa bandari wa Izmir, Uturuki, ikiwa ni miaka 40 tangu safari ya mwisho kama hiyo kufanyika.

Kwa mujibu wa shirika la habari la AFP, Libya haijapata huduma za ferry za kimataifa kwa takriban miaka 25. Safari za baharini pamoja na zile za ndani nchini humo zilitatizika kuanzia mwaka 2011 baada ya mapinduzi yaliyomuondoa kiongozi wa muda mrefu Moamer Kadhafi, pamoja na ghasia zilizofuata.

Wakati wa utawala wa Kadhafi,kuanzia 1969, taifa hilo lilikuwa chini ya vikwazo, ambavyo viliathiri pakubwa shughuli za kitalii. Safari za ferry zitakazo chukua saa 48 kufika Uturuki, sasa zimefufuliwa tena na kampuni ya Libya ya Kavalay, wakati ferry iliyoanza safari ikitarajiwa kurejea Libya hapo Decemba 7.

Taha Hadid ambaye ni afisa kwenye bandari ya Misrata amesema kwamba wanakusudia kuanza tena safari za meli kuelekea Misri na Tunisia. Mji huo ambao ni watatu kwa ukubwa nchini Libya uko takriban kilomita 200 mashariki mwa Tripoli, wakati ukisemekana kuwa na wafanyabiashara wengi kutoka Uturuki.

XS
SM
MD
LG