Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumamosi, Aprili 20, 2024 Local time: 15:31

Joto kali ni tishio kwa jamii zinazoishi mijini - Utafiti


Watu wanavyokabiliana na msimu wa joto kali Spain. (Picha na AP).
Watu wanavyokabiliana na msimu wa joto kali Spain. (Picha na AP).

Shirika la Utabiri wa Hali ya Hewa Duniani lilitangaza mwaka 2019 kuwa ni moja ya  miaka iliyokuwa na joto lililopindukia ulimwenguni ukilinganisha na hali ilivyokuwa tangu mwaka  1850.

Ongezeko la hali ya joto duniani na wimbi la joto linaweza kufanya maeneo ya mijini yenye idadi kubwa ya watu kuwa haikaliki, utafiti mpya unaonyesha.

Shirika la Utabiri wa Hali ya Hewa Duniani lilitangaza mwaka 2019 kuwa ni moja ya miaka iliyokuwa na joto lililopindukia ulimwenguni ukilinganisha na hali ilivyokuwa tangu mwaka 1850.

Kote barani Afrika, maeneo yenye joto zaidi yamehusishwa na maeneo ya mijini kutokana na shughuli muhimu za kiuchumi zinazofanyika humo na watu wanaoishi katika miji hiyo, timu ya wanasayansi wa Kichina walisema.

Wanasayansi hao wanasema joto kali zaidi limeshuhudiwa kati ya Novemba na Machi, huku asilimia 60 ya eneo la ardhi barani Afrika limeathiriwa.

Na katika ukanda Kusini kumekuwa na siku 24 za matukio ya ongezeko la joto huku viwango vya joto vikiongezeka kwa digrii tatu za celsius na katika eneo la kaskazini, kwa siku nane viwango vya joto viliongezeka kwa digrii 1.8.

Watafiti hao walieleza hatari zinazo ongezeka kutokana na matukio ya joto katika maeneo ya mijini yenye wakazi wengi zaidi, na kutahadharisha kuwa maeneo haya yenye hali hii yanaweza kuwa vigumu kwa watu kuishi ikifikapo mwisho wa karne.

“Maeneo yenye joto zaidi yalihusishwa na idadi kubwa ya watu mijini, hususan pwani ya magharibi, kaskazini mashariki, kusini na eneo la ikweta huko Afrika, ambako idadi kubwa ya wakazi wanaishi,” wanasayansi hao kutoka Taasisi ya Atmospheric Physics, Chinese Academy of Sciences walisema katika chapisho lao la Machi 9.

XS
SM
MD
LG