Upatikanaji viungo

Breaking News
Alhamisi, Aprili 25, 2024 Local time: 10:02

Mkutano wa mazingira wa UNEP wafunguliwa Nairobi


Wajumbe wa UNEP wakiwa kwenye mkutano wa awali. Picha ya maktaba
Wajumbe wa UNEP wakiwa kwenye mkutano wa awali. Picha ya maktaba

Shirika la mazingira la Umoja wa Mataifa UNEP Jumatatu limefungua kikao chake cha 5 kuhusu mazingira mjini Nairobi wakati zaidi ya mataifa 100 yakitarajiwa kushiriki na kuzungumzia hatua za kwanza kuweka mkataba wa kimataifa wa kukabiliana na tatizo la plastiki ulimwenguni.

Akihutubia kikao hicho cha ufunguzi Katibu mkuu wa Umja wa Mataifa Antonio Guterres amewashambulia vikali viongozi wa mataifa makuu ya dunia kutokana na kutoonyesha uongozi katika kukabiliana na mabadiliko ya hali ya hewa ulimwenguni.

Viongozi wa kimataifa wakiwemo mawaziri wa mazingira wanakutana hapo Nairobi pamoja na wale wanaohudhudhuria kwa njia ya kimitandao, ili kubuni kamati itakayoshugulikia mkataba huo ndani ya kipindi cha miaka miwili ijayo. Zaidi ya mataifa 50, wanasayansi pamoja, makampuni pamoja na wanaharakati wa mazingira wametoa sauti yao kuhusu umuhimu wa kuweka kanuni kali za kukabiliana na tatizo la plastiki kwenye mazingira.

Moja wapo ya mapendekezo ni kudhibiti idadi ya utoaji wa bidhaa hizo zinazotengenezwa kwa kutumia mafuta na gesi, wakati wadadisi wakikisia kwamba utoaji wake huenda ukaongezeka maradufu kufikia mwaka wa 2040. Mataifa yanayozalisha plastiki kwa wingi kama vile Marekani na China yameonekana kuunga mkono hatua hiyo, ingawa hayajaelezea mikakati inayohitajika katika kukabiliana na tatizo hilo

XS
SM
MD
LG