Merkel mwenye umri wa miaka 67, amepewa heshima ya juu inayotolewa na jeshi kwa raia.
Kiongozi huyo alizaliwa katika mji wa bandari wa Hamburg, kaskazini mwa Ujerumani na wazazi wake walihamia sehemu za mashariki alipokuwa mdogo na kuongoza chama cha Christian Democratic Party, CDU, baada ya muungano wa nchi yake.
Baada ya miaka 16 ofisini, nafasi ya Merkel itachukuliwa wiki ijayo na Olaf Scholz.
Merkel ameiongoza Ujerumani na Ulaya kukabiliana na migogoro kadhaa, na amekuwa mtetezi wa demokrasia wakati kuna ongezeko la uongozi wa kiimla kote duniani.
Wakosoaji wake hata hivyo wanasema kwamba alisimamia matatizo badala ya kuyatatua, na kwamba mrithi wake atatakiwa kufanya maamuzi magumu anapoingia ofisini.