Upatikanaji viungo

Breaking News
Ijumaa, Aprili 19, 2024 Local time: 16:26

Mvutano waghubika mchakato wa kuunda serikali mpya Ujerumani


Aliyekuwa chansela wa ujerumani Angela Merkel akinwya maji wakati wa mojawapo ya vikao vya bunge akiwa bado madarakani.
Aliyekuwa chansela wa ujerumani Angela Merkel akinwya maji wakati wa mojawapo ya vikao vya bunge akiwa bado madarakani.

Juhudi za vyama vya ujerumani kuunda serikali mpya kuchukua nafasi ya muungano wa Angela Merkel zimekumbana na changamoto kadhaa, na kupelekea juhudi zao za kutaka kumchagua chansela mpya mwezi ujao kukumbwa na hali ya sintofahamu.

Chama cha wademokrat wa mrengo wa kati kikiongozwa na Olaf Scholz, kiliibuka katika nafasi ya mbele kuunda serikali mpya baada uchaguzi wa kihistoria wa mwezi Septemba uliopelekea kuchindwa kwa chama cha waconservative cha Angela Markel.

Mgawanyiko umetokea katika mazungumzo kati ya chama cha mazingira na wademokrat walio huru FDP, katika juhudi za kuunda serikali ya muungano.

Maswala ya uekezaji katika mazingira, hali ya baadaye ya muungano huo na uteuzi wa Waziri wa fedha ndiyo yamesababisha mgawanyiko.

Iwapo vyama hivyo vitashindwa kufikia makubaliano kabla mwisho wa mwezi huu, hatua ya kumchagua chansela Olaf Scholz itachelewa.

XS
SM
MD
LG