Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumatano, Julai 17, 2024 Local time: 20:06

Jeshi la Syria lashambulia ngome ya waasi Idlib


Bashar al Assad
Bashar al Assad

Utawala wa Syria umefyatua makombora yaliyoua raia saba wakiwemo watoto watatu katika ngome kuu ya mwisho ya waasi ya Idlib, taasisi inayofuatilia masuala ya vita yenye makao yake Uingereza ilisema hii leo.

Makombora yalipiga katika Kijiji cha Ehsim, Jumamosi jioni kusini mwa mkoa wa Idlib, kituo kinachofuatilia haki za binadamu Syria, kimeeleza.

Mwanafamilia mmoja aliliambia shirika la Habari la AFP, kuwa wageni walikusanyika kumpongeza ndugu wa kiume kwa kuoa, wakati tukio hilo lilipotokea nyumbani kwao.

Mapema Jumapili, makombora yaliyofyatuliwa na vikosi vinavyoiunga mkono serikali, yaliua raia katika kijiji cha Sarja, wakiwemo watoto watatu na mfanyakazi mmoja wa uokozi.

Jumla ya watu waliouawa katika shambulizi hili wamefikia jumla ya watu 13 huko Idlib.

Mashambulizi huko Ehsim, yalikuja saa kadhaa baada ya Rais Bashar al-Assad, kula kiapo cha uongozi kwa muhula wa nne, akiahidi kukomboa maeneo ambayo bado hayako katika udhibiti wa serikali.

Chanzo cha habari : AFP

XS
SM
MD
LG