Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumatatu, Julai 22, 2024 Local time: 19:46

Watu 13 walikufa wakijaribu kuchota mafuta baada ya lori la mafuta kupinduka


Watu wakishuhudia lori la mafuta lililopata ajali na kuungua huko Kenya
Watu wakishuhudia lori la mafuta lililopata ajali na kuungua huko Kenya

Watazamaji walikimbilia eneo la tukio wakiwa na madumu ya kubeba mafuta lakini lori lililipuka na kuwaathiri wale waliokuwa karibu na hapo wakichota mafuta alisema Charles Chacha, mkuu wa polisi katika kaunti ya Siaya, mahala ambapo ajali iliyokea

Polisi nchini Kenya walisema Jumapili kwamba watu 13 waliuawa na wengine wengi waliungua vibaya na moto wakati gari lililobeba petroli lilipopinduka na kusababisha mlipuko huko magharibi mwa Kenya huku umati wa watu ukifurika kuchota mafuta yaliyomwagika.

Lori la mafuta liligongana na gari jingine na kupinduka Jumamosi karibu na Malanga umbali wa kilomita 315 kaskazini-magharibi mwa Nairobi kwenye barabara kuu yenye shughuli nyingi kati ya Kisumu na mpaka wa Uganda.

Watazamaji walikimbilia eneo la tukio wakiwa na madumu ya kubeba mafuta lakini lori lililipuka na kuwaathiri wale waliokuwa karibu na hapo wakichota mafuta. "Lililipuka na kuwaka moto wakati watu wakichota mafuta yaliyokuwa yakitiririka", alisema Charles Chacha, mkuu wa polisi katika kaunti ya Siaya, mahala ambapo ajali iliyokea.

Wafanyakazi wa zimamoto walifika kwenye eneo la tukio saa mbili baadae kuzima moto wakati wale waliojeruhiwa katika mlipuko huo walipelekwa hospitali. "Wengine wengi wamepelekwa hospitali wakiwa na majeraha mabaya, wakiwemo watoto wadogo", Chacha alisema.

Sababu ya mlipuko huo bado haijajulikana.

XS
SM
MD
LG