Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumanne, Aprili 16, 2024 Local time: 17:42

Jaji wa Texas asitisha mpango wa DACA unaowalinda wahamiaji vijana kurudishwa makwao


Program ya DACA ambayo inawalinda wahamiaji vijana kurudishwa nchi walizotoka
Program ya DACA ambayo inawalinda wahamiaji vijana kurudishwa nchi walizotoka

Walalamikaji wameapa kukata rufaa juu ya uamuzi huo wa jaji wa wilaya, Andrew Hanen ambaye alitangaza program inayojulikana kama DACA ni kinyume cha sheria akizuia serikali kuidhinisha  maombi yeyote mapya lakini anaiacha program hiyo kama ilivyo kwa waombaji waliopo

Wanaharakati Marekani wanawasihi wa-Democrat na Rais Joe Biden kuchukua hatua haraka juu ya sheria ya kuwalinda wahamiaji vijana baada ya jaji wa serikali kuu katika jimbo la Texas, alipoamuru Ijumaa kufuta program ya enzi ya Obama, ambayo inalinda kufukuzwa kwa maelfu ya wahamiaji walioletwa Marekani wakiwa watoto.

Walalamikaji wameapa kukata rufaa juu ya uamuzi huo wa jaji wa wilaya, Andrew Hanen ambaye alitangaza program inayojulikana kama DACA ni kinyume cha sheria akizuia serikali kuidhinisha maombi yeyote mapya lakini anaiacha program hiyo kama ilivyo kwa waombaji waliopo.

Akiita uamuzi huo kuwa “wakati wa kupaza sauti” kwa wa-Democrat mkurugenzi mtendaji wa “United We Dream” Greisa Martinez Rosas, alisema watalaumiwa tu kama mageuzi ya sheria hayatafanyika.

Hanen alitoa uamuzi huo akiipendelea Taxas na majimbo manane mengine ya ki-Conservative ambayo yalishtaki ili kusitisha mpango wa DACA ambao unatoa ulinzi kwa watu 650,000.

XS
SM
MD
LG