Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumatano, Desemba 07, 2022 Local time: 19:28

Mwanamichezo kutoka Uganda azamia kwenye Olympic Japan


Logo ya michezo ya Olympic huko Tokyo 2020 ambayo iliahirishwa hadi 2021 kutokana na janga la Corona.

Julius Ssekitoleko aligundulika hayupo kutoka eneo la mazoezi la timu ya Uganda huko Izumisano mji uliopo Osaka magharibi mwa Japan

Mwanamichezo raia wa Uganda aliyepotea kutoka kwenye kambi ya mazoezi ya Olympic hapo Ijumaa aliacha barua inayosema anataka kuendelea kukaa Japan vyombo vya habari vilisema na kuongeza mkanganyiko kabla ya michezo ambayo inaanza wiki ijayo.

Julius Ssekitoleko aligundulika hayupo kutoka eneo la mazoezi la timu ya Uganda huko Izumisano mji uliopo Osaka magharibi mwa Japan.

Ripoti za vyombo vya habari zilisema Ssekitoleko aliacha barua inayosema anataka kuendelea kukaa na kufanya kazi nchini Japan kwani maisha huko Uganda yalikuwa magumu. Ssekitoleko hakuwa amehitimu kushiriki katika michezo ya Tokyo na alitakiwa kurudi Uganda Jumanne ijayo.

Facebook Forum

XS
SM
MD
LG