Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumanne, Februari 07, 2023 Local time: 15:10

Jeshi la Somalia lakamata udhibiti wa vijiji kadhaa muhimu kijeshi kutoka kwa al-Shabab


Picha iliyotolew na jeshi la Marekani Februari 12, 2021 ikionyesha rundo la silaha aina mbalaimbali zikiwemo bunduki aina ya Kalashnikov na makombora yenye mabomu yaliyokamatwa katika meli inayosafirisha kwa magendo silaha hizo katika pwani ya Somalia.

Wizara ya Ulinzi ya Somalia inasema jeshi la taifa la nchi hiyo, likisaidiwa na wanamgambo wa koo, wamekamata udhibiti wa vijiji kadhaa muhimu kiusalama kutoka kwa wanamgambo wa Kiislam wa al-Shabab.

Wizara hiyo imekiri kwamba wana usalama kadhaa walijeruhiwa wakati wa operesheni hiyo ya karibuni ya kijeshi.

Abdullahi Ali Anod, msemaji wa Wizara ya Ulinzi ya Somalia, ambaye alizungumza na waandishi wa habari Jumamosi katika mji mkuu Mogadishu, alisema jeshi, likisaidiwa na wenyeji katika maeneo hayo, walikamata vijiji vinne vya kimkakati kutoka kwa kundi la wanamgambo la al-Shabab lenye uhusiano na al-Qaida.

Vijiji viliyokombolewa ni Gulane, Darusalam, Harga-Dhere na Mabah, ambavyo viko katika mikoa ya Hiran na Middle Shabelle.

Mabah ni Kijiji cha mwisho mashariki wa Hiran ambacho kilikuwa chini ya udhibiti wa al-Shabab, kwa mujibu wa shirika la habari la Somalia linaloendeshwa na serikali la Sonna.

Anod alisema wapiganaji sita wa al-Shabab waliuawa katika mkoa wa Middle Shabelle, wakati 10 waliuawa wakati wa mapambano kati ya jeshi la kundi hilo ambayo yalifanyika katika mkoa wa Hiran.

Alikiri kwamba wanajeshi watatu wa serikali walijeruhiwa wakati wa operesheni za karibuni; akiongezea kwamba walikomboa zaidi ya kilometa 80 kutoka kwa al-Shabab.

Alisema wanajeshi wawili kati ya watatu walikuwa na majeraha makubwa sana.

Anasema watui walikuwa wakiuliza kwanini juhudi zinazofanyika zinachukua muda mrefu sana. Ni kwasababu ya mapigano ya msituni. Siyo vita vya kijeshi, na jeshi lazima liwafurushe wote na kuwaondoa kutoka maeneo ya ndani ya nchi, ambapo operesheni inachukua muda.

Vijiji ambavyo viko karibu na kiini cha mapigano dhidi ya al-Shababm, katika jimbo Hirshabele.

Siku chache zilizopita, mamlaka ya Somalia ilisema takriban magaidi 40 wa al-Shabab waliuawa, na wengine kadhaa kujeruhiwa, katika operesheni mpya katika mkoa wa Middle Shabelle nchini Somali.

Ghasia zilianza baada ya al-Shaba kuushambulia msafara uliobeba misaada muhimu ya chakula iliyokuwa inahitajika, kuchoma magari moto na kuua takriban watu 20, wakiwemo wasafiri.

Kundi hilo lilizidisha mashambulizi yake baada ya Rais wa Somalia, Hassan Sheikh Mohamud, kuchaguliwa mwezi Mei mwaka huu na kutangaza “vita kamili”: dhidi ya wanamgambo.

Waziri Mkuu wa Somalia Hamza Abdi Barre wiki iliyopita alisema kuwa operesheni ya ulinzi imepeleka kuuawa kwa wapiganaji 600 wa al-Shabab na wengine 1,200 kujeruhiwa katika muda wa miezi mitatu iliyopita.

Facebook Forum

XS
SM
MD
LG