Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumanne, Oktoba 08, 2024 Local time: 21:36

Marekani yawawekea vikwazo watu 8 wanaoshukiwa kujihusisha na ugaidi


FILE - Ijumaa, Feb. 12, 2021, Picha hii imetolewa na Jeshi la Majini la Marekani ikionyesha silaha mbalimbali zilizokamatwa zikisafirishwa kwa magendo katika pwani ya Somalia.
FILE - Ijumaa, Feb. 12, 2021, Picha hii imetolewa na Jeshi la Majini la Marekani ikionyesha silaha mbalimbali zilizokamatwa zikisafirishwa kwa magendo katika pwani ya Somalia.

Serikali ya Marekani inajaribu kuzuia mtiririko wa silaha kwa washirika wa kikundi cha kigaidi cha Islamic State nchini Somalia, wakilenga operesheni za magendo ya silaha.

Operesheni hizi pia zinasaidia kumpa silaha hasimu wake mwenye Marekani mwenye uhusiano na al-Qaida, kundi la al-Shabaab, zikiwemo silaha kutoka Iran.

Wizara ya Fedha ya Marekani Jumanne ilitangaza vikwazo dhidi ya watu binafsi nane na kampuni moja zote zikihusishwa katika juhudi za mwaka mzima za ulanguzi wa silaha zenye thamani ya mamilioni ya dola kati ya Yemen na Somalia.

Kati ya wale wanaolengwa ni Abdirahman Fahiye, anayeaminika kuongoza operesheni za kila siku za IS- Somalia, Mohamed Ahmed Qahiye, anayeongoza kitengo cha ujasusi cha IS- Somalia na Isse Mohamoud Yusuf, haramia wa zamani ambaye anaendelea kusafirisha silaha kwa niaba ya IS.

Vikwazo hivyo “vinaelekezwa moja kwa moja kwa mtandao unaofadhili na kusambaza kwa vikundi vyote viwili vya ISIS-Somalia na al-Shabab,” Brian Nelson, waziri mdogo wa ugaidi na utalii wa kifedha, alisema katika taarifa yake, akitumia herufi za mkato nyingine kwa mshirika wa IS.

Wapiganaji wa Al-Shabab wakionesha silaha zao wakiwa wanafanya mazowezi yao kaskazini ya Mogadishu
Wapiganaji wa Al-Shabab wakionesha silaha zao wakiwa wanafanya mazowezi yao kaskazini ya Mogadishu

“Kuhusika kwa wale waliotajwa [Jumanne] katika harakati nyingine za kihalifu, ikiwemo uharamia na uvuvi haramu, kunaonyesha kwa kiwango gani ISIS – Somalia ina muingiliano na mitandao ya kihalifu na jumuiya nyingine za kigaidi zinazo endesha shughuli zake katika kanda hiyo,” Nelson alisema.

Hatua hiyo iliyochukuliwa Jumanne na Wizara ya Fedha inafuatia duru ya vikwazo vya awali vilivyowekwa mwezi uliopita, vikikusudia kudhoofisha uwezo wa al-Shabab kuchangisha fedha.

Vikwazo hivyo vipya, hata hivyo, vinajikita kwa viongozi wawanaofanya magendo na ugaidi ambao niwashiriki katika kikundi cha IS-Somalia, licha ya mafungamano ya sasa au ya zamani na al-Shabab, uhusiano wa zamani na washirika wa al-Qaida huko Yemen au uhusiano na Iran.

“Sidhani ni kitu chochote cha kiitikadi,” Caleb Weiss, mchambuzi mwandamizi wa Taasisi ya Kulinda Demokrasia na Taasisi ya Bridgeway, aliiambia VOA kwa njia ya barua pepe.

“Wanatumia mitandao ile ile ya magendo na wafanya magendo ambao wanafurahia kufanya biashara na yule anayetoa bei ya juu,” Weiss alisema. “Nina uhakika kuwa Iran pia inaangalia hili kama ni fursa ya kujipatia fedha zaidi, pia.”

Kulingana na maafisa wa Wizara ya Fedha wa Marekani, hii imeendelea kuwa biashara kubwa.

XS
SM
MD
LG