Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumamosi, Desemba 10, 2022 Local time: 02:00

Jeshi la Marekani lawaua waasi wawili wa Al-Shabaab nchini Somalia


Vikosi vya Somalia msituni vikijiandaa kupambana na kundi la kigaidi la al-Shabaab.

Shambulizi la angani la jeshi la Marekani limewalenga waasi wa al-Shabab waliokuwa wakishambulia vikosi vya Jeshi la Taifa la Somalia, na kuwaua wawili kati yao, kwa mujibu wa Kamandi ya Marekani barani Afrika (AFRICOM).

Shambulzi hilo la Jumapili lilifanyika karibu na mji wa Buulo-barde, nchini Somalia, kilomita 218 kaskazini magharibi mwa mji mkuu, Mogadishu.

AFRICOM inasema tathmini yake ya awali ni kwamba magaidi wawili waliokuwa wakishambulia vikosi vya Somalia waliuawa, na kwamba hakuna raia aliyejeruhiwa au kuuawa.

"Al-Shabab ndio mtandao mkubwa zaidi, na wenye nguvu zaidi wa al-Qaida duniani, na umethibitisha nia na uwezo wake wa kushambulia vikosi vya Marekani na kutishia maslahi ya usalama ya Marekani," kamandi hiyo ilisema katika taarifa Jumanne, na kuongeza kuwa itaendelea "kuchukua hatua za kuzuia kundi hilo la kigaidi, lenye nia mbaya, ya kupanga na kufanya mashambulizi, dhidi ya raia."

Shambulio hilo la Marekani limefanyika wakati ambapo al-Shabab wamefanya mashambulizi mawili makubwa nchini Somalia mwezi huu.

Shambulizi katika Hoteli ya Tawakal, siku ya Jumapili, katika mji wa pwani wa kusini wa Kismayo, lilisababisha vifo vya watu wasiopungua 11, na mwanzoni mwa Oktoba, shambulio la mabomu matatu katika mji wa Bele-dweyne, liliua takriban watu 20.

Facebook Forum

XS
SM
MD
LG