Upatikanaji viungo

Breaking News
Ijumaa, Desemba 08, 2023 Local time: 02:16

Watu 20 wauwawa  na 36 kujeruhiwa na kundi la Al Shabab Somalia


Kundi la wanamgambo wa Alshabab Somalia.
Kundi la wanamgambo wa Alshabab Somalia.

Wapiganaji wa Kiislamu wenye itikadi kali siku ya Jumatatu walilenga makao makuu ya serikali ya Somalia katika eneo la Hiran, na kuuwa watu 20  na kujeruhi wengine 36.

Hayo yalitokea katika mji ulio katikati ya harakati za hivi karibuni dhidi ya wanamgambo wenye itikadi kali, maafisa na mashahidi walisema.

Kundi la al-Shabab lenye makao yake nchini Somalia lilidai kuhusika na shambulio hilo huko Beledweyne, mji ulio umbali wa zaidi ya kilomita 300 kaskazini mwa mji mkuu wa Somalia, Mogadishu.

Serikali ya Somalia mapema Jumatatu ilitangaza kwamba ikiwa na washirika wa kimataifa wamemuua kiongozi mkuu wa al-Shabab, Abdullahi Nadir, mwishoni mwa juma. Jeshi la Marekani lilisema lilifanya shambulizi la anga siku ya Jumamosi kusini magharibi mwa Somalia lakini halikumtaja kiongozi wa al-Shabab aliyeuawa.

Gavana wa Hiran, Ali Jayte Osman, ambaye alinusurika katika shambulio la Jumatatu, aliambia Associated Press kwamba waziri wa afya wa jimbo la Hirshabelle na naibu gavana wa Hiran anayesimamia fedha ni miongoni mwa waliouawa katika shambulio la Jumatatu. Takriban watu wengine 36 walijeruhiwa.

XS
SM
MD
LG