Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumamosi, Aprili 20, 2024 Local time: 20:37

Jenerali Powell aaga dunia akiwa na umri wa miaka 84


Hayati Jenerali Colin Powell (AP Photo/Sait Serkan Gurbuz)
Hayati Jenerali Colin Powell (AP Photo/Sait Serkan Gurbuz)

Jenerali Colin Powell, mtu Mweusi wa kwanza kushikilia wadhifa wa Waziri wa Mambo ya Nje wa Marekani na aliyekuwa mwenyekiti wa Wakuu wa Vikosi vya pamoja vya jeshi , amefariki Jumatatu kutokana na matatizo ya COVID-19. Alikuwa na umri wa miaka 84.

Familia yake imetangaza kifo chake kupitia Ukurusa wa Facebook, wakisema, “Tumempoteza mtu muhimu, mume mpenzi, baba, babu na Mmarekani shupavu.”

Familia hiyo imesema kuwa Powell alipata chanjo kamili dhidi ya virusi vya corona na kuwashukuru wafanyakazi wa hospitali katika Kituo cha Matibabu cha Taifa cha Walter Reed nje ya Washington “kwa kumpa huduma nzuri” wakati wa siku zake za mwisho.

Powell alikuwa mwanadiplomasia wa ngazi ya juu nchini kutoka mwaka 2001 hadi 2005 wakati wa awamu ya kwanza ya Rais wa Republikan George W. Bush.

Kabla ya hapo, Powell, Jenerali wa Jeshi mwenye nyota nne na shujaa aliyehudumu kwa miaka 35, alikuwa kiongozi wa kijeshi wa Wizara ya Ulinzi, mwenyekiti wa wakuu wa majeshi, kutoka 1989 hadi 1983, chini ya baba ya Bush, Rais George H.W. Bush.

XS
SM
MD
LG