Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumapili, Desemba 04, 2022 Local time: 22:45

Gbagbo azindua chama kipya cha siasa


Aliyekuwa rais wa Ivory Coast Laurent Gbagbo

Aliyekuwa rais wa Ivory Coast Laurent Gbagbo Jumapili amezindua chama kipya cha kisiasa kwa matarajio kwamba kitamrejesha madarakani tena.

Gbagbo ambaye amekuwa uhamishoni mwa muongo mmoja amezindua chama hicho kwa jina African People’s Party wakati akilenga kuunganisha mrengo wa kushoto na kutumia nafasi hiyo kushinda kwenye uchaguzi wa 2025.

Kwa mujibu wa shirika la habari la AFP, Gbagbo ameambia wajumbe wa chama chake kwamba sasa wameanza safari mpya pamoja kabla ya kuhutubia umati mkubwa wa wafuasi wake, ikiwa mara ya kwanza tangu kurejea kwake nchini kati kati mwa mwezi Juni. Gbagbo ameongeza kuwaambia wafuasi wake kwamba atabaki mwanasiasa hadi kufa.

Ripoti zinaongeza kusema kwamba waakilishi kutoka vyama vya kisiasa kutoka mataifa kadhaa ya kiafrika walihudhuria hafla hiyo. Gbagbo mwenye umri wa miaka 76 alitawala Ivory Coast kati ya 2000 na 2011 wakati kukiwa na misukasuko na migawanyiko ya kisiasa kwenye taifa hilo linaloongoza kwenye uzalishaji wa cocoa ulimwenguni.

Kiongozi huyo aliondolewa madarakani Aprili 2011 baada ya vita vya wenyewe kwa wenyewe vilivyoua takriban watu 3,000. Ghasia hizo zilichochewa na hatua yake ya kukatalia madarakani hata baada ya kushindwa kwenye uchaguzi na rais wa sasa Alassane Ouattara.

Facebook Forum

XS
SM
MD
LG