Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumapili, Juni 16, 2024 Local time: 15:07

Mgogoro wa kisiasa waongezeka Sudan kati ya viongozi wa chama tawala


Baraza la Mawaziri la Sudan lakutana Khartoum. (Photo by - / Office of Sudan's Prime Minister / AFP) /
Baraza la Mawaziri la Sudan lakutana Khartoum. (Photo by - / Office of Sudan's Prime Minister / AFP) /

Baraza la Mawaziri la Sudan linakutana Jumatatu katika kikao cha dharura wakati mgogoro wa kisiasa ukiendelea kuongezeka nchini humo kati ya viongozi wa chama kinachotawala cha uhuru na mabadiliko – FFC.

Waandamanaji wanaounga mkono jeshi la Sudan wameendelea na maandamano kwa siku ya tatu mfululizo, wakiongeza joto la shinikizo ambalo Waziri Mkuu Abdalla Hamdok ametaja kama mgogoro mbaya na hatari sana kwa mabadiliko ya utawala wa nchi hiyo.

Waandamanaji wamekusanyika nje ya makao makuu ya rais mjini Khartoum, wakiitaka serikali ya mpito kuvunjiliwa mbali kwa madai kwamba imekosa kutekeleza wajibu wake kisiasa na kiuchumi kwa manufaa ya raia wa Sudan.

Maandamano yanatokea wakati siasa za Sudan zinajaribu kujitoa katika mgawanyiko uliotokea baada ya kuangushwa kwa utawala wa Omar al-Bashir.

Waandamanaji wanaounga mkono serikali nao wanapanga kuandamana kesho Jumanne.

XS
SM
MD
LG