Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumanne, Juni 17, 2025 Local time: 05:12

Jaribio la kuipindua serikali ya Sudan limezimwa - Maafisa


Waandamanaji wa kupinga utawala wa Sudan wakipeperusha bendera ya nchi hiyo mjini mwaka wa 2019.
Waandamanaji wa kupinga utawala wa Sudan wakipeperusha bendera ya nchi hiyo mjini mwaka wa 2019.

Vyombo vya habari vya serikali nchini Sudan vinaripoti kwamba jaribio la mapinduzi lililofanyika mapema Jumanne limeshindwa.

"Kumekuwa na jaribio la mapinduzi lililoshindwa, watu wanapaswa kukabiliana nalo," vyombo vya habari vinavyomilikiwa na serikali viliripoti.

Chanzo cha ngazi ya juu cha serikali kilisema kwamba wale waliopanga njama walijaribu kuchukua udhibiti wa jengo la shirika la utangazaji la kitaifa "walishindwa."

Chanzo kingine cha ngazi ya juu cha kijeshi kilisema kundi la maafisa "walihusika katika jaribio hilo lakini walisimamishwa mara moja."

Mapema Jumanne, iliripotiwa kuwa vifaru vilipita mbele ya hospitali ya jeshi katika mji wa Omdurman na kufunga barabara kuelekea daraja la zamani la Omdurman, karibu na bunge la Sudan, wakati kukishuhudiwa uwepo mkubwa wa vikosi vya jeshi katika eneo hilo.

Vikosi vya usalama vya Sudan hata hivyo vilifunga daraja kuu ya kuvuka mto Nile, na ambayo linaunganisha miji ya Khartoum na Omdurman.

Muhammad al-Faki Suleiman, mwanachama wa Baraza Kuu la Sudan na msemaji rasmi wa Baraza hilo, alitoa wito kwa Wasudan wote "kuitetea nchi yao."

XS
SM
MD
LG