Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumapili, Desemba 10, 2023 Local time: 20:31

Maandamano yafanyika ikulu ya Sudan yakidai iondoke serikali yenye njaa


Maandamano Sudan
Maandamano Sudan

Makundi ya kijeshi na raia yamekuwa yakishirikiana madaraka katika nchi hiyo ya Afrika mashariki katika muungano ambao si rahisi  tangu kuondolewa madarakani kwa Rais wa muda mrefu Omar al- Bashir mwaka 2019

Maelfu ya waandamanaji walioshikamana na jeshi walikusanyika mbele ya makazi ya Rais mjini Khartoum leo Jumamosi, wakiimba “Iondoke serikali yenye njaa” wakati Sudan inapambana na mzozo mkubwa wa kisiasa katika kipindi chake cha mpito cha miaka miwili.

Makundi ya kijeshi na raia yamekuwa yakishirikiana madaraka katika nchi hiyo ya Afrika mashariki katika muungano ambao si rahisi tangu kuondolewa madarakani kwa Rais wa muda mrefu Omar al- Bashir mwaka 2019. Lakini kufuatia jaribio la mapinduzi lililoshindwa mwezi Septemba lililohusishwa na vikosi vitiifu kwa Bashir, viongozi wa jeshi wamekuwa wakidai mageuzi katika ushirika wanaouita, “Forces of Freedom and Change (FFC) na baraza la mawaziri la raia.

Hata hivyo viongozi wa kiraia wanawashutumu FFC kwa lengo la kunyakua madaraka. Kikundi kilichojiweka pamoja jeshi cha FFC pamoja na vikundi vyenye silaha ambavyo viliasi dhidi ya Bashir viliitisha maandamano ya Jumamosi.

XS
SM
MD
LG