Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumapili, Julai 14, 2024 Local time: 13:22

Jaji Mkuu wa Kenya adai serikali inataka kumuondoa madarakani


Rais Uhuru Kenyatta akipongezwa na Jaji Mkuu David Maraga baada ya kuapishwa Nairobi, Kenya Novemba 28, 2017. REUTERS/Baz Ratner
Rais Uhuru Kenyatta akipongezwa na Jaji Mkuu David Maraga baada ya kuapishwa Nairobi, Kenya Novemba 28, 2017. REUTERS/Baz Ratner

Jaji Mkuu wa Kenya David Maraga amejitokeza kueleza vizuizi vinavyoikabili ofisi yake na mhimili wa mahakama nzima ukinyanyaswa na mhimili wa serikali unaoongozwa na Rais Uhuru Kenyatta.

Gazeti la The East African nchini Kenya limeandika Jumatatu kuwa Maraga aliyeonekana akiwa na hasira, katika hotuba yake aliyoitoa kupitia televisheni kwa taifa, akiwa katika jengo la Mahakama ya Juu mjini Nairobi Jumatatu.

Jaji Mkuu amefichua madai ya hujuma ya siri inayofanywa na viongozi wa serikali kumuondoa madarakani kabla ya kufika Disemba 31, 2019.

“Baadhi ya Mawaziri wanasema nitaondolewa kabla ya kufika mwisho wa mwaka, kumbe hii Kenya ina wenyewe?” Jaji Maraga, akitabasamu baadhi ya wakati alipokuwa anahutubia, alisema.

Aliishutumu Hazina ya Taifa bila ya haki kuendelea kuzilenga mahakama katika hatua yake ya kubana matumizi wakati bajeti za Bunge na Serikali zikiendelea kuongezwa.

“Jaji Mkuu hana gari aina ya Mercedes, tuliambiwa ni ufujaji wa fedha, wakati Maspika wawili wa bunge la taifa wanazo,” alisema wakati akieleza jinsi alivyolazimishwa kukubaliana na hali hiyo, na hivyo kutoweza kuwapa usafiri wakiwemo wageni wake Majaji Wakuu ambao wanahitaji usafiri.

Tangia mwaka 2014, bajeti ya mahakama hiyo imekuwa ikipunguzwa na mwaka huu, imepokea kiwango kisichoweza kusaidia cha asilimia 0.69 ya bajeti ya taifa.

XS
SM
MD
LG