Upatikanaji viungo

Breaking News
Ijumaa, Aprili 19, 2024 Local time: 10:19

Amnesty International yasema Mahakama ya Juu Kenya imetekeleza Katiba


Rais Uhuru Kenyatta akizungumza baada ya kutangazwa kubatilishwa kwa uchaguzi wa urais
Rais Uhuru Kenyatta akizungumza baada ya kutangazwa kubatilishwa kwa uchaguzi wa urais

Watu wengi wanafikiria kuwa mahakama Kenya ziko huru na kwa uamuzi huu wa kubatilisha matokeo ya uchaguzi wa urais ambapo Rais Uhuru Kenyatta alitangazwa kuwa mshindi wameonyesha mfano kwa dunia nzima.

Katika tamko lake mkurugenzi wa shirika la haki za binadamu Kenya (Amnesty International) amesema kuwa mahakama imeonyesha kuwa iko huru na itakuwa ni mfano wa kuigwa na nchi nyingine duniani.

Wakati uamuzi huo wa mahakama “ umetekeleza katiba iliokuwa imepitishwa mwaka 2010, “utadadisi jukumu la waangalizi wa uchaguzi, ambao kwa pamoja wamesema kuwa uchaguzi ulifanyika vizuri,” mwanadiplomasia mmoja wa Afrika ameliambia shirika la habari la AFP kwa sharti jina lake lisitajwe.

Vyanzo vya habari nchini Kenya vimesema kuwa katika jumla ya maamuzi yaliyofikiwa na mahakama, Jaji Maraga amesema kuwa Tume Huru ya Uchaguzi na Mipaka (IEBC) ilikuwa imehusika katika ukiukwaji wa katiba na dosari zilizojitokeza katika uchaguzi ambazo zimeathiri ukweli wa matokeo hayo.

Lakini mpaka ripoti kamili ya uamuzi wa mahakama itapotolewa, haiko wazi uamuzi huo umejikita katika kitu gani.

“Wamefikia moja ya uamuzi muhimu katika historia ya Kenya,” Amesema Cheeseman, “ na mpaka baada ya siku 21 tutaweza kujua ni kwa nini uamuzi huo ulifikiwa.”

Wachambuzi wamesikitishwa na kusubiriwa uamuzi huo wakisema kuwa tamko la mahakama la mwisho linauwezekano mkubwa wa kushawishi kura zitakazoopigwa wakati uchaguzi unaporudiwa na watu ambao watakuwa na jukumu la kusimamia uchaguzi huo.

“Sababu moja iliyopelekea uchaguzi huu kuwa na mapungufu ilikuwa ni muda mdogo wa kutekeleza zoezi la uchaguzi waliopewa IEBC,” Cheeseman amesema, akiongeza kuwa makamishna wapya walitangazwa miezi saba kabla ya uchaguzi uliofanyika mwezi Agosti.

“Na hivi sasa muda ni mchache zaidi kwa maandalizi hayo.”

Kwa upande wake, mwanadiplomasia ambaye hakutaka jina lake litajwe amesema Kenya inaweza kuona mfumuko wa kero nyingine kutoka kwa wagombea ambao wamepoteza nafasi za ugavana, useneta na ubunge katika kinyanganyiro hicho wakienda mahakamani na malalamiko ya uchaguzi kufuatia maamuzi ya mahakama hiyo.

“Watu wengi wataendelea kuwa na wasiwasi,” Cheeseman amesema. “Wakenya wametoka hivi karibuni tu kwenye uchaguzi wenye utata, na maamuzi haya ya mahakama yanaisukuma nchi hiyo kwenda katika kampeni upya za uchaguzi, ambazo zitaanzo mara moja.”

“Matokeo ya uchaguzi unaorudiwa unaweza ukagubikwa na migogoro tena.”

XS
SM
MD
LG