Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumamosi, Aprili 20, 2024 Local time: 05:55

Mabalozi Kenya wasema uamuzi wa mahakama ni mfano kwa dunia


Balozi wa Marekani nchini Kenya Robert Godec
Balozi wa Marekani nchini Kenya Robert Godec

Mabalozi wa nchi za nje Kenya wamesema uamuzi wa Mahakama ya Juu kubatilisha ushindi wa Rais Uhuru Kenyatta “ni mfano kwa Afrika na ulimwengu.”

Katika tamko la pamoja walilolituma kwa vyombo vya habari masaa mawili baada ya uamuzi wa mahakama saa tano asubuhi na kusainiwa na mabalozi wote, pia wamechukua fursa hiyo kuwapongeza watu wa Kenya kwa "kuonyesha uvumilivu na kujiamini” katika mfumo wa sheria wa nchi hiyo.

Hakuna uchaguzi wa urais ambao umewahi kubatilishwa kabla ya hapo.

“Taasisi za uchaguzi Kenya inalazimika kuanza maandalizi ya uchaguzi wa mpya wa urais baadae mwaka huu na kuwahimiza kila mtu kuhakikisha kuwa uchaguzi ni huru, haki, wakweli na amani.Tunaimani kuwa Kenya na raia wake wanauwezo wa kufikia hayo,” limesema tamko hilo.

Katika maamuzi yaliyotolewa na mahakama Ijumaa, Mahakama imesema kuwa bodi ya uchaguzi haukufuata katiba na uchaguzi ulikuwa na kasoro wakati wa upigaji kura mwezi uliopita, ambao umeathiri ukweli wa uchaguzi.

Mahakama pia imeamrisha kuwa uchaguzi mwengine ufanyike katika kipindi cha siku 60.

XS
SM
MD
LG