Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumatano, Oktoba 04, 2023 Local time: 15:13

Islamic State yadai kushambulia zahanati mjini Lume, DRC na kuua watu 14


PICHA YA MAKTABA: Mashambulizi ya mara kwa mara mashariki mwa DRC yanasabisha wasiwasi mwingi kati ya wakazi.

Kundi la kigaidi la Islamic State limedai kutekeleza shambulio la siku ya Alhamisi ambalo lililenga mji wa Lume, jimbo la Kivu Kaskazini, mashariki mwa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo, kwa mujibu wa ujumbe wa shirika la habari la kundi hilo.

Kundi hilo limedai kuhusika kupitia taarifa kwenye mtandao wa Telegram bila kutoa maelezo zidi.

Siku ya Ijumaa, mashahidi wawili walisema washambuliaji waliwaua zaidi ya dazeni moja ya watu katika zahanati moja, na kusema uvamizi huo ulitekelezwa na wapiganaji wa Kiislamu wanaoshirikiana na Islamic State.

Kundi hilo lilishambulia kliniki inayoendeshwa na kanisa katika majira ya saa nne usiku wa Alhamisi.

Msemaji wa jeshi Alinukiwa akisema kwamba washambuliaji hao wanatoka katika kundi ambalo linashirikiana na kundi la ADF na kwamba walikuwa wabnatumia mbinu zinanzowiana na zile zinazotumiwa na kundi hilo.

Jeshi liliwaua wapiganaji hao watatu na kumkamata mmjoja baada ya kujibu shambulizi hilo katika mji wa Lume, alisema msemaji wa jeshi Antony Mualushay.

XS
SM
MD
LG