Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumapili, Juni 16, 2024 Local time: 16:35

Marekani : Idara za Serikali zaanza kutoa huduma, wafanyakazi kuharakishiwa malipo


Mfanyakazi wa usimamizi wa usafiri akimrudishia kitambulisho msafiri baada ya kukihakiki Jan. 25, 2019, Uwanja wa ndege wa Kimataifa wa Seattle-Tacoma huko Seattle.
Mfanyakazi wa usimamizi wa usafiri akimrudishia kitambulisho msafiri baada ya kukihakiki Jan. 25, 2019, Uwanja wa ndege wa Kimataifa wa Seattle-Tacoma huko Seattle.

Baadhi ya idara mbalimbali za serikali ya Marekani zilizo kuwa zimefungwa kwa siku 35 zimefunguliwa Jumamosi, siku mbili kabla ya Idara ya Mapato ya Ndani (IRS) kuanza kushughulikia mchakato wa kupokea mawasilisho ya kodi za wananchi kwa mwaka 2018.

Kufungwa kwa serikali kulifikia tamati siku ya Ijumaa usiku, baada ya Rais Donald Trump kusaini muswada wa matumizi ya wiki tatu uliopitishwa na Bunge kumaliza kufungwa kwa serikali kuliko chukuwa muda mrefu zaidi kuliko wakati wowote mwengine katika historia ya Marekani.

Takriban wafanyakazi wa serikali kuu 800,000 walikosa kulipata mishahara yao kwa mara ya pili siku ya Ijumaa. Mapema wiki hii, Bunge la Marekani lilipitisha na Trump alisaini sheria inayoagiza idara za serikali kuu kuwalipa wafanyakazi mishahara iliyokuwa haijalipwa “kwa haraka itakavyo wezekana.”

Lakini maafisa wa serikali wametahadharisha kuwa inaweza kuchukua siku kadhaa kwa wafanyakazi wa serikali kuu kupata malipo yao yote waliokuwa hawajalipwa.

Ofisi ya Utawala na Bajeti ya Marekani ilituma waraka jioni Ijumaa kwa idara na ofisi za serikali zilizo kuwa zimefungwa kuwajulisha kuwa vitengo vyao sasa vimefunguliwa na kuwa wafanyakazi wao wanaweza kurejea kazini.

Waraka huo pia ulizitaka idara hizo “kufungua ofisi hizo tena mara moja na kwa kufuata utaratibu.”

Ujumbe kwa wafanyakazi wote wa idara ya kodi ya ndani uliyokuwa katika tovuti yao ulisema wafanyakazi wanatarajiwa kuripoti kazini masaa manne baada ya tangazo hilo kupostiwa siku ya Ijumaa, Januari 25, 2019, saa tat una nusu usiku saa za ukanda wa mashariki, Marekani.”

Na zaidi ya hilo, tangazo hilo liliwashauri wafanyakazi “kuripoti kazini kwa mujibu wa kuanza kwa ratiba inayofuatia ya siku yako ya kazi.”

XS
SM
MD
LG