Upatikanaji viungo

Breaking News
Ijumaa, Machi 29, 2024 Local time: 14:45

Kufungwa kwa serikali kuu Marekani kumeweka historia


Jengo la bunge Marekani linavyoonekana wakati serikali kuu imefungwa
Jengo la bunge Marekani linavyoonekana wakati serikali kuu imefungwa

Ikiwa katika siku yake ya 22 bado hakuna mwangaza ni lini serikali kuu Marekani itafunguliwa. Hatua hii imetokana na mvutano kati ya Rais Trump na bunge ambapo rais anadai apatiwe fedha za ujenzi wa ukuta kwenye mpaka wa Marekani na Mexico na bunge linakataa

Kufungwa kwa baadhi ya huduma za serikali kuu Marekani kumeingia katika vitabu vya historia siku ya Jumamosi katika siku yake ya 22 na kuwa tukio lililochukua muda mrefu sana kwenye historia ya Marekani. Kufungwa kwa serikali kuu kulitokana na mvutano baina ya Rais Donald Trump na bunge kuhusu mabilioni ya dola anayotaka rais kwa ajili ya ujenzi wa ukuta kwenye mpaka wa Marekani na Mexico.

Siku ya Ijumaa Rais Trump aliita hali kwenye mpaka wa Marekani na Mexico ni uvamizi lakini baadae alisema hatotangaza hali ya dharura ya kitaifa kwa wakati huu kama njia ya kupata fedha kwa ajili ya ujenzi wa ukuta na kumaliza kufungwa kwa baadhi ya huduma za serikali kuu.

Rais Donald Trump
Rais Donald Trump

Katika matamshi yake Rais Trump ya karibuni juu ya kutoelewana na wabunge wa Democrats kufuatia ombi lake la takribani dola bilioni tano za fedha za awali kwa ujenzi wa uzio wa kudumu kwenye mpaka Trump alisema angependa kuona bunge la Marekani linapiga kura na kuidhinisha fedha hizo.

Rais Trump ambaye anatoka chama cha Republican alieleza “kile ambacho hatuna nia ya kukifanywa kwa hivi sasa ni hali ya dharura ya kitaifa”. Shughuli nyingi za serikali kuu Marekani zilifungwa Disemba 22 mwaka jana baada ya fedha za matumizi kumalizika.

XS
SM
MD
LG