Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumanne, Aprili 23, 2024 Local time: 22:24

Trump atakutana tena na wabunge kujadili kufunguliwa serikali kuu


Spika wa bunge Nancy Pelosi alimshutumu Trump "kuishikilia mateka" serikali kuu kutokana na ahadi yake ya kampeni ya kujenga ukuta kwenye mpaka wa Marekani na Mexico ambapo alidai Mexico wangelipia gharama za ukuta

Rais wa Marekani Donald Trump amewaalika viongozi wa bunge kutoka vyama vyote kwa mkutano mwingine huko White House siku ya Ijumaa kuzungumzia jinsi ya kumaliza kufungwa kwa serikali kuu ambayo inakaribia kuingia wiki yake ya tatu.

Mazungumzo yaliofanyika Jumatano hayakusonga mbele baada ya pande zote kushindwa kufikia muafaka wakati Rais Trump akitaka apewe dola bilioni tano za ujenzi wa ukuta kwenye mpaka wa Marekani na Mexico na wademocrat wanasema hawampi hata senti moja.

Spika wa bunge la Marekani, Nancy Pelosi
Spika wa bunge la Marekani, Nancy Pelosi

Spika wa bunge mdemocrat Nancy Pelosi alikiambia kituo cha TV cha NBC cha Marekani “tunaweza kwenda mbele na kurudi nyuma. Ni mara ngapi zaidi inabidi tuseme hapana, hakuna fedha kwa ajili ya ujenzi wa ukuta”. Pelosi alimshutumu Trump kuishikilia mateka serikali kuu kufuatia ahadi yake ya kampeni ya kujenga ukuta ambapo alidai Mexico wangelipia gharama za ukuta.

Pelosi alipanga kuwasilishwa miswada miwili bungeni Alhamis usiku, mmoja wa kutoa fedha kwa serikali nzima hadi Septemba ikiwemo idara ambazo zimefungwa hivi sasa na mwingine kutoa fedha kwa idara ya usalama wa ndani hadi Februari 8.

Miswada hii itafungua tena serikali kuu na kuendelea na mjadala wa fedha kwa ajili ya ujenzi wa ukuta. Kiongozi wa baraza la seneti mrepublican Mitch McConnell alisema miswada ya bunge haitakwenda popote na ni mchezo wa kisiasa.

XS
SM
MD
LG