Wafanyakazi wa FBI kwa mara ya kwanza Ijumaa hii hawatopata mishahara yao, wakati leo ikiwa ni siku ya 20 baadhi ya idara za serikali kuu zikiwa zimefungwa kutokana na mvutano kati ya Rais DonaldTrump na Wademocrats juu ya ujenzi wa ukuta kwenye eneo la mpaka kati ya marekani na Mexico.
“Hali imekuwa mbaya sana, kazi muhimu inayo fanywa na FBI inahitaji pesa”, umesema umoja huo unaowakilisha wafanyakazi elfu 13, katika malalamiko waliyo wailisha jana kwenye bunge na white House.
Tangu shughuli ya baadhi ya idara za serekali kuu kufungwa hapo Disemba 22, baadhi ya wafanyakazi laki 8 wa serikali kuu walilazimika kukaa nyumbani, wengine waliendelea kufanya kazi bila kulipwa mishahara, miongoni mwa hao kuna wafanyakazi elfu 5 wa FBI.