Wizara ya afya inasema kumekuwa na watu 34 wanaodhaniwa wameambukizwa na virusi hivyo vya hatari.
Inaamini kwamba watu 21 wamefariki kutokana na Ebola.
Jopo la wataalamu wa afya linaendelea kuwatafuta watu wowote waliokutana na waathiriwa wa ugonjwa huo.
Mlipuko ulianza katika wilaya ya kati ya Mubende, lakini sasa umeenea katika wilaya mbili jirani.
Hakuna kesi yoyote iliyothibitishwa katika mji mkuu wa Kampala. Huu ni mlipuko wa nne kutokea Uganda.
Nchi jirani zimesema ziko katika hali ya tahadhari kubwa.