Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumapili, Desemba 10, 2023 Local time: 20:46

Vifo vya Ebola nchini Uganda vyaongezeka na kufikia vinne


Waziri wa afya wa Uganda Diana Atwine akithibitisha kisa cha kwanza cha Ebola nchini humo, katika mkutano wa waandishi wa habari mjini Kampala, Septemba 20, 2022. Picha ya AP
Waziri wa afya wa Uganda Diana Atwine akithibitisha kisa cha kwanza cha Ebola nchini humo, katika mkutano wa waandishi wa habari mjini Kampala, Septemba 20, 2022. Picha ya AP

Wagonjwa wengine watatu wa Ebola wamefariki nchini Uganda, wizara ya afya imesema Ijumaa, na kufikisha idadi ya vifo kuwa vinne, siku kadhaa baada ya maafisa kuthibitisha mlipuko wa aina mpya ya ugonjwa huo mbaya ambao chanjo yake haijaidhinishwa bado.

Wizara ya afya ya Uganda ilithibitisha watu 11 wameambukizwa na virusi vya Ebola pamoja na vifo vinne.

Mlipuko wa sasa ambao unahusishwa na aina nadra ya virusi vya Ebola inayopatikana Sudan, ulianzia katika kijiji kidogo cha wilaya ya Mubende mwanzoni mwa mwezi huu wa Septemba, maafisa wamesema.

Vifo vingine saba vinachunguzwa kwa kuhusishwa na mlipuko wa Mubende, wilaya inayopatikana umbali wa kilomita 130 mashariki mwa mji mkuu Kampala.

Kifo cha kwanza kilikuwa cha mwanaume wa miaka 24 ambaye alifariki mapema wiki hii.

XS
SM
MD
LG